GGML WANG'ARA MAONESHO YA SABASABA, WAIBUKA MUAJIRI BORA

KAMPUNI ya Geita Gold Mine Limited (GGML), imeendelea kung'ara baada ya kuibuka mshindi katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara - Dar es Salaam maarufu kama sabasaba kwa kunyakua tuzo ya muajiri bora na msafirishaji bora wa madini nje ya nchi.


Pia GGML imepata tuzo ya mlipa kodi bora wa pili na muajiri bora anayezingatia taratibu za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).


 Tuzo zote zimetolewa Julai 13 na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango ( wa pili kulia) na kupokewa na Mwanasheria Mwandamizi wa GGML, David Nzaligo (wa pili kushoto waliosimama nyuma) kwa niaba ya uongozi wa kampuni. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments