MNARA WA KUMBUKUMBU YA VIONGOZI WA DINI WALIOFANYA KAZI KUBWA YA KUENEZA INJILI WAZINDULIWA KIGOMA...WAONYWA KUTUMIA DINI KAMA KICHAKA CHA MAOVU - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Sunday, July 17, 2022

MNARA WA KUMBUKUMBU YA VIONGOZI WA DINI WALIOFANYA KAZI KUBWA YA KUENEZA INJILI WAZINDULIWA KIGOMA...WAONYWA KUTUMIA DINI KAMA KICHAKA CHA MAOVU


Mnara wa kumbukumbu ya viongozi wa dini waliofanya kazi kubwa ya kueneza injili mkoani Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (Kulia) kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mnara wa kumbukumbu ya viongozi wa dini waliofanya kazi kubwa ya kueneza injili mkoani Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (Kulia) kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mnara wa kumbukumbu ya viongozi wa dini waliofanya kazi kubwa ya kueneza injili mkoani Kigoma.
Askofu Msaidizi wa kanisa la Pentekoste Motomoto la mjini Kigoma Mathias Bwami (kulia) akiongoza waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini ya kikristo kufanya usafi kwenye hospitali teule ya Babtisti mjini Kigoma ikiwa sehemu ya uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya viongozi wa dini waliofanya kazi kubwa ya kueneza injili mkoani Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (wa tatu kushoto) akisalimiana na maaskofu na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya kikristo mkoani Kigoma alipowasilia eneo la Katonga Manispaa ya Kigoma Ujiji kuzindua mnara wa kumbukumbu ya viongozi wa dini waliofanya kazi kubwa ya kueneza injili mkoani Kigoma.
Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAKAMU wa Raisi Dk.Philip Mpango amewaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini kuacha kutumia shughuli za dini kama kichaka cha kufanya maovu na mwenendo unaokwenda kinyume na maadili ya Mtanzania na kwamba serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wote wa dini watakaobainika kuwa na mwenendo huo.

Makamu wa Raisi alisema hayo akizindua mnara wa kumbukumbu ya viongozi wa dini wa madhehebu ya kikristo waliofanya kazi kubwa ya kueneza injili mkoani Kigoma.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa viongozi wa dini kupitia madhehebu yao wamefanya kazi kuleta maendeleo chanya kwenye jamii pamoja na kuhudumia roho za waumini hivyo kuleta amani na utulivu kwenye jamii.

Makamu wa Raisi katika hotuba yake hiyo alisema kuwa Taasisi za dini zimechochea mabadiliko makubwa kwenye suala zima la maendeleo hasa kwenye Nyanja za elimu, afya na kilimo na kwamba serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za dini kama mdau mkubwa wa maendeleo.

“Pamoja na hayo dini hazipaswi kutumika kama kichaka cha kuficha uchafu na mwenendo unaokwenda kinyume na maadili ya Tanzania, kwa sababu hiyo serikali itaendelea kuchukua hatua stahiki dhidi na taasisi za dini watakaokiuka sheria,”Alisema Makamu wa Raisi katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa mkoa Kigoma.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Pan African Christian Foundation for Evangelization Assistance (PACFEA), Jared Mlongecha alisema kuwa uzinduzi wa mnara huo umelenga kutambua kazi kubwa ya viongozi hao wa dini wa madhehebu mbalimbali ya kikristo katika kueneza injili ya neon la Mungu.

Mlongecha alisema kuwa neno la Mungu limekuwa na mchango mkubwa katika kuijenga jamii kuwa na tabia na mwenendo mwema katika kuleta ustawi,amani, umoja na mshikamano miiongoni mwa wanadamu.

Pamoja na kueneza Injili ya neno la Mungu Mkurugenzi huyo alisema kuwa taasisi hiyo imejikita katika kusaidia watu wasiojiweza ili kuleta uwiaono wa maisha kwa watu wote na kwa kuwatumia marafiki zao kutoka maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Marekani itawafikia watu wenye uhitaji katika kuwapatia mahitaji muhimu ya kibinadamu.

Uzinduzi huo wa mnara ambao ulitanguliwa na mahubiri ya neno la Mungu kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre ulihudhuriwa na maaskofu kutoka nchi za Marekani, Zambia,Malawi na Zibwabwe ambapo hafla hiyo pia iliambatana na viongozi na waumini kufanya usafi kwenye hospitali Teule ya Babtisti iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mjini Kigoma.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages