OJADACT YALAANI MAUAJI YA WATOTO GEITA

 


TAMKO  LA  KULAANI MAUAJI YA WATOTO MKOANI GEITA, JUNI   22 2022

OJADACT  inalaani  matukio  ya  mauaji  yanayoendelea  Nchini  husasani  matukio  mawili  ya  mauaji  ya  watoto  yaliyotokea  Mkoani  Geita,  tukio la kwanza  lilihusisha  kifo  cha  aliyekuwa  Mwanafunzi wa Darasa  la saba  Johson  Thomas (14) katika  shule  ya Msingi Buhalahala , Halmashauri  ya Mji  Geita, Mkoa wa Geita, aliyekutwa  amefariki na mwili wake ukiwa pembeni  mwa Mto baada  ya kupotea Juni 2, 2022.


Tukio la pili ni  tukio la  kuuawa kwa mtoto  Dorcas Mathias  mwenye  umri  wa  Miaka (7)  aliyekuwa  Mwanafunzi wa Chekechea Shule ya Msingi Ibambi Wilaya ya Nyahg’wale Mkoani Geita  baada ya  kuvamiwa na watu  watatu  wakati akiwa  aanachunga  mbuzi na  mwenzake.


Kamanda  wa Polisi  Mkoani Geita Henry Mwaibambe alisema  baada  ya  mwili huo kufanyiwa  uchunguzi na Daktari alibainika  kuwa,Dorcas alibakwa, kulawitiwa na kisha  kuuawa na  baadaye akavunjwa  shingo. Jeshi  la Polisi  limewafikisha  Mahakamani watuhumiwa   watatu Mathias Shilole (52),Mganga wa tiba  asili na Mkazi waKilimanajro Nyangwale na  LucyMdelema kwa tuhuma za kujihususha  na mauaji  hayo.


OJADACT imebaini sababu mbalimbali za  maujai   hayo  ni  pamoja na 


1.Imani  za kishirikina  kwenye  jamii zinahusishwa na  kujipatia utajiri kwa njia nyepesi


2.Ukatili kwenye jamii  unaombatana  na malezi mabaya  ya  jamii  isiyo na  staha


OJADACT  inatoa  rai  kwa  jamii  kutojihusisha na   vitendo  vya  uvunjifu wa  sheria na badala  yake jamii iwe  mlinzi wa mtoto kwa kutoa tarifa  inapoona  viashiria  vya  ukiukwaji wa haki za mtoto ikiwemo haki ya  kuishi.

 Serikali na wadau  mbalimbali wanendelee  kufanya kazi  kwa pamoja  ya kumlinda mtoto.          

 Edwin Soko

 Mwenyekiti

 OJADACT

22.06.2022

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments