TGNP, UNFPA WAENDESHA MDAHALO NA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI NYIKOBOKO KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA..VIJANA WAANIKA SABABU ZA MDONDOKO SHULENI


Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akizungumza wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la UNFPA kwa ufadhili wa KOICA wamefanya mdahalo/ majadiliano na vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii lengo likiwa ni kuongeza ushiriki wa vijana/wavulana katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na mdondoko mkubwa wa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari.

Akizungumza wakati wa mdahalo huo leo Alhamisi Juni 9,2022 katika kijiji cha Shilela kata ya Shilela, Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina amesema majadiliano hayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wananchi kiuchumi katika halmashauri ya Msalala unaotekelezwa na TGNP kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la UNFPA kwa ufadhili wa KOICA.

“Tumekutana na wanafunzi wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko kwa lengo la kuongeza ufahamu na ushiriki wa vijana wa kiume katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia mashuleni na ndani ya jamii. Tumewapa mbinu za kulinda watoto wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa kuhakikisha wanazuia ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa za matukio na viashiria vya ukatili wa kijinsia”,amesema Joyce.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga amesema vijana wa kiume wana nafasi kubwa ya kulinda watoto wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa kuhakikisha wanazuia ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa kwa wazazi, walimu ama viongozi waliopo kwenye maeneo yao.

“Vijana wa kiume ninyi ni askari kulinda na kusaidia dada zenu, usimuache dada yako afanyiwe ukatili,hakikisha unatoa taarifa kwa mtu wa karibu anayeweza kutatua tatizo akiwemo mwalimu au mzazi wako. Tunataka kuona wanafunzi waliojisajili kidato cha kwanza, darasa la kwanza wamalize masomo wakiwa idadi ile ile, hatutaki kuona mdondoko wa wanafunzi shuleni”,amesema.

Kwa upande wake, Mwalimu Mlezi wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko, John Banda amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 299 na kwa upande wa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2022 ni 43 licha ya kwamba walisajiliwa 172 kidato cha kwanza, wengine hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuhama,mimba na utoro sugu.

Wakizungumza wakati wa majadiliano hayo, wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko wamesema bado kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaendelea katika jamii ikiwemo mimba na ndoa za utotoni, wanawake kupigwa na waume zao,wazazi kutowapa watoto wa kike muda wa kujisomea,wazazi kuzuia wanafunzi wa kike kufanya vizuri kwenye mitihani ili wafeli waolewe.

Wanafunzi hao wamebainisha kuwa kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia zimekuwa zikikwama au kutoripotiwa kutokana na imani za kishirikina “Baadhi ya watu wanashindwa kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kutokana na hofu ya kurogwa na wahusika wanaotenda ukatili…Ukifuatilia sana unaweza kupuliziwa dawa hivyo wanaona ni bora kila mtu apambane na hali yake”, hivyo elimu bado inahitajika sana ili kukomesha ukatili wa kijinsia.

Aidha wamezitaja miongoni mwa sababu zinazosababisha wanafunzi kuacha shule (mdondoko) ni pamoja na hali ngumu kiuchumi unaosababisha wakose uwezo wa kuwahudumia watoto/wanafunzi matokeo yake wanafunzi wanaamua kuacha shule ili wakatafute maisha.

“Pia tamaa ya wazazi kupata mali wanaamua kumwachisha masomo mtoto wa kike aolewe apate mahari. Lakini kukosekana kwa ajira baada ya kumaliza masomo ni sababu nyingine inayofanya wanafunzi waache shule. Wananchi wanasema huku mtaani kuwa watu wengi wamesoma lakini hawana ajira..Sasa nyumbani maisha magumu halafu niende shule kufanya nini wakati hata nikisoma kupata ajira ina vigumu si bora nikapambane tu na hali yangu mtaani”,amesema Yudas Michael.

Naye Dickson Robert amesema adhabu zinazotolewa na walimu kwa makosa ya kinidhamu zinasababisha baadhi ya wanafunzi kukimbia shule kutokana na kushindwa kuvulimia maisha ya shule huku akiongeza kuwa uwezo mdogo wa wanafunzi darasani unawafanya baadhi yao kukimbia shule.

Kwa upande wake, Lucas Justine ameeleza kuwa utoro sugu wa wanafunzi unaosababishwa na wazazi kutojali maisha ya wanafunzi ‘kuchukulia poa’ ni chanzo kingine cha mdondoko wa wanafunzi shuleni hali inayochangiwa pia na wanafunzi kujiunga na makundi ya vijana wa mtaani.

Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela Joseph Mbunge amesema sasa kuna mabadiliko katika jamii ambapo wananchi wanatoa taarifa kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia hivyo ili kuokoa jamii vijana wa kiume wanayo nafasi kuelimisha wenzao kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia na wawe wanatoa taarifa kwa walimu walezi na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa na viongozi wa serikali.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akizungumza leo Alhamisi Juni 9,2022 wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii. Mdahalo huo uliongozwa na mada ya 'Mambo gani yanasababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni' umeandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la UNFPA kwa ufadhili wa KOICA. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akizungumza wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii. 
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP,Bi. Joyce Mkina akizungumza leo Alhamisi Juni 9,2022 wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii. Mdahalo huo uliongozwa na mada ya 'Mambo gani yanasababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni'
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii. 
Mwalimu Mlezi wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko, John Banda akizungumza wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii. 
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko, Emmanuel Shija Maganga akichangia hoja wakati wa mdahalo kuhusu mambo yanayochangia mdondoko wa wanafunzi shuleni. Kulia ni Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina.
Wanafunzi wakifuatilia mjadala kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Yudas Michael akichangia hoja wakati wa mdahalo kuhusu mambo yanayochangia mdondoko wa wanafunzi shuleni. Kushoto ni Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina  
Lucas Justine akichangia hoja wakati wa mdahalo kuhusu mambo yanayochangia mdondoko wa wanafunzi shuleni. Kulia ni Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina  
Wanafunzi wakifuatilia majadala
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko wakifanya majadiliano kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko wakifanya majadiliano kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko wakifanya majadiliano kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko wakifanya majadiliano kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyikoboko wakifanya majadiliano kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Dickson Robert akiwasilisha kazi ya kikundi chake kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Bleze John akiwasilisha kazi ya kikundi chake kuhusu mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Yudas Michael (kulia) akielezea mambo yanayosababisha mdondoko wa wanafunzi shuleni
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa kituo cha taarifa na maarifa Shilela wakifuatilia mjadala
Msaidizi wa Kisheria Gridius Gration kutoka shirika la DEMAO akielezea mbinu za kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela Joseph Mbunge akielezea shughuli zinazofanywa na vituo vya taarifa na maarifa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa kijiji cha Shilela Charles Shiminzi Ngeleja akizungumza wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii. 
Afisa Mtendaji wa kata ya Shilela, Mwanaidi Mustapha akizungumza wakati akifunga majadiliano na vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Nyikoboko iliyopo katika kata ya Shilela halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii  
Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post