MWANAMKE ALIYEUAWA KWA KUPIGWA MAWE KUZIKWA KESHO KITETO


Angel Mwaisumwa, aliyeuawa kwa kupigwa mawe
**
Mwanamke aitwaye Angel Mwaisumwa, aliyeuawa na wananchi kumpiga mawe Juni 10, 2022, wilayani Kiteto kwa tuhuma za kununua viungo vya binadamu atazikwa Jumatatu katika Kijiji cha Matui wilayani humo baada ya familia yake kushindwa kumsafirisha kwenda kwao Mbeya.


Familia ya Angel imeeleza kwamba imefikia uamuzi huo kwa kuwa hawana uwezo wa fedha wa kusafirisha mwili hadi mkoani Mbeya.

Hadi sasa jumla ya watu 15 wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa kuhusishwa na tukio la mauaji ya mwanamke huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post