WANAOUZA NGONO WHATSAPP, FACEBOOK WADAKWA DARJeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam imewakamata watu wawili kwa tuhuma za usambazaji wa picha za ngono na kuuza mwili kwa njia ya Mtandao ya kijamii ikiwemo facebook, WhatsApp, Tinder na Exotic tz.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam Murilo Jumanne amesema watuhimiwa hao ni Marry Samson Sibora maarufu Asha Zungu ( 23), Mzanaki, mkazi wa Sinza Mugabe na Zainabu Yahaya Omary maarufu official Manka ( 23), Mrangi, mkazi wa Buguruni.


Kamanda Muliro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na Timu maalum ya kuzuia na kupambana na uhalifu mtandaoni, ambayo imefanya Oparesheni maalum kuanzia May 18,2022 hadi June 26,2022 na wamehojiwa kwa kina na taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe Mahakani haraka iwezekanavyo.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, linatoa onyo kali kwa watu wanao jihusisha na uhalifu kwa njia ya mtandao na njia nyingine, kuwa Serikali na vyombo vyake imejipanga kupambana na uhalifu wa aina yoyote, na wahalifu popote walipo watafuatwa, kukamatwa na kupelekwa Mahakamani”

“Aidha, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Watanzania wote kutumia mitandao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kuwa waangalifu na vitendo vya utapeli, ikiwemo kuchukuwa tahadhari wakati wa kutuma pesa au kufanya biashara katika mitandao ili kuepuka kutapeliwa, pia watu wajiepushe kufanya biashara haramu mitandaoni kama vile za kuuza mili na ngono” amesem Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM Muliro Jumanne Muliro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post