AKAMATWA KWA KUTUMIA WANAFUNZI WA DARASA LA SITA KUFUKUA KABURI
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Rukwa ACP Theopita Mallya
**
Tanda Thadeo ambaye ni mkazi wa Sumbawanga mkoani Rukwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuwatumia wanafunzi wa Darasa la sita shule ya msingi Kasisiwe iliyopo Manispaa ya Sumbawanga kushiriki zoezi la kufukua kaburi la mtoto ili afufuliwe na baba yake kwa kuwalipa shilingi elfu kumi.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Rukwa ACP Theopita Mallya amethibitisha kuwa jeshi hilo linamshikilia Tanda Thadeo mwenye miaka 30 mkazi wa kitongoji cha Kasisiwe kilichopo manispaa ya Sumbawanga kwa tuhuma za kuwatumia wanafunzi hao kwa madai ya kumfufua mwanae hali ambayo imempelekea Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa kuitembelea shule hiyo na kutoa elimu kwa wanafunzi ya kutambua matendo ya kihalifu.

Hata hivyo Marry Kway ambaye ni kamanda wa Jeshi la Polisi wilaya ya Sumbawanga naye alikuwepo kwa ajili ya kutoa somo la ukatili wa kijinsia na namna ya kuripoti matukio ya kiharifu kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kupunguza vitendo vya uvunjifu wa amani kwa jamii.


Mtoto huyo aliyefariki mwenye umri wa miaka miwili alijulikana kwa jina la Martine Tanda na alizikwa 17.6.2022 kidini kwenye makaburi ya kitongoji cha Kasisiwe.

Chanzo - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments