Breaking : OLE SABAYA NA WENZAKE WAACHIWA HURU



Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya ushahidi uliotolewa na jamhuri kugubikwa na utata, hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Juni 10 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.


Hii ni kesi ya pili Sabaya kushinda ambapo Mei 6, 2022 na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, walishinda rufaa iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, waliyokata kupinga hukumu ya miaka 30 iliyokuwa imetolewa na na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.


Hakimu Kisinda amesema kuwa mbali na sababu hizo,mahakama imegundua kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu na kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yao mahakamani hapo haujaweza kuthibitisha mashtaka hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments