KIJANA MBARONI TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MITANOKISA NG'OMBE

Mtuhumiwa aliahidiwa akikamilisha unyama huo atapewa Ng’ombe watatu kama malipo
***
KIJANA mmoja anayefahamika kwa jina la Juma Jackson (30) mkazi wa Kijiji cha Kagunga wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kumbaka na kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo akiwa anatoka nyumbani kwao kuelekea mji wa jirani.

“Alimvutia vichakani kisha kumvua nguo zake na kuanza kumbaka na kumlawiti huku akimkaba shingo na kumuamru asipige kelele,” amesema Makame.

Kwa mujibu wa ACP Makame, uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina, aliahidiwa kulipwa ng’ombe watatu baada ya kutekeleza kitendo hicho na mtu (jina limehifadhiwa).


“Walikubaliana baada ya kufanya unyama huo aende akamuogeshe shambani kwake ili iwe kama zindiko kwa ajili ya shamba,” amefafanua Makame.

“Tulimkamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa wazazi wa mtoto, alifanya ukatili huo Mei 13, 2022 saa 12:00 jioni, anaendelea kuhojiwa tukikamilisha upelelezi tutamfikisha mahakamani,” amesema Makame

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post