YANGA SC YAENDELEA KUSONGA MBELE, YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Sunday, May 15, 2022

YANGA SC YAENDELEA KUSONGA MBELE, YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0


***********************

Na Alex Sonna-DODOMA

BAADA ya kucheza mechi tatu bila kupata ushindi hatimaye vinara Yanga wameng’ara ugenini kwa kuichapa Dodoma jiji Mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Yanga walianza mpira kwa kushambulia kwa kasi yake na katika dakika ya 11 Dickson Ambundo aliwanyanyua mashabiki wake baada ya kufunga bao nzuri kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Dodoma.

Licha ya kupata bao Yanga waliendelea kulishambulia lango la wenyeji na mnamo dakika ya 35 Golikipa wa Dodoma jiji Mohammed Yusuph alijifunga baada ya shuti la Zawadi Mauya.

Mnamo dakika ya 87 Dodoma jiji walipata pigo baada ya kiungo wake Hassan Maulid kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu Yannick Bangala.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 60 wakiwa wanahitaji Pointi 11 waweze kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu wakiwa wamebakiwa na Mechi 6 mkononi nafasi ya pili wapo Simba wakiwa na Pointi 49 huku wakiwa wamebakiwa mechi 7.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages