RAIS SAMIA APOKEA TUZO YA HESHIMA NCHINI GHANA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor tarehe 25 Mei 2022 Accra nchini Ghana.


RAIS Samia anapokea tuzo ya mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye kwa mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo hutolewa kwa Mkuu wa nchi iliyofanya vizuri.


Baada ya kupokea tuzo hiyo Rais Samia amesema anajisikia faraja kwa kuwa Rais wa Kwanza Mwanamke Barani Afrika kupokea tuzo hiyo kwani ni heshima kwake na heshima kwa kile anachokifanya katika nchi yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor tarehe 25 Mei 20220 Accra nchini Ghana.


Rais Samia amesema suala la utekelezaji wa miundombinu ni mchakato endelevu ambao umeanza tangu awamu ya kwanza ya muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Julius Nyerere lakini lilishika hatamu zaidi katika awamu ya nne ya utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao uliendelea hadi kufikia katia awamu yake na ni mengi yamefanyika kuhusu suala la miundombinu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor tarehe 25 Mei 20220 Accra nchini Ghana.



Ameongeza kwa kusema ili Bara la Afrika liweze kujikomboa kiuchumia miundombinu ni jambo mtambuka na lazima lipewe kipaumbele ili liwweze kusaidia kukuza uchumi wa Afrika.


Rais Samia amebainisha kuwa 60% ya ardhi iliyopo Afrika inafaa kwa kilimo achilia mbali rasilimali nyingine zilizopo kama vle madini pamoja na utalii vyote hivi ili viweze kuwa na tija basi miundombinu mizuri lazima iwepo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor pamoja na viongozi mbalimbali wa Benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara.


Kwa upande mwingine Rais Samia ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Tanzania katika kuboresha miundombinu nchini, akisistiza kuwa anajisikia mwenye faraja kubwa kwa kufanikiwa kukamilisha baadhi ya miradi mikubwa ya miundombinu ndani ya muda mfupi wa utawala wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments