WANAUME MURUFITI WALIA KUNYANYASWA NA WAKE ZAO , WATAKA MADAWATI YA KUWATETEA


Wananchi wa kijiji cha Murufiti na viongozi wakiwa kwenye kongamano la kupinga ukatili na unyanyasaji kijinsia lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia tanzania (TGNP) lililofanyika kijiji cha Murufiti wiayani Kasulu mkoani Kigoma.

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Baadhi ya wanaume walioshiriki mjadala wa kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia wameomba kuanzishwa kwa dawati litakaloshughulikia utetezi kwa wanaume kutokana na manyanyaso na vipigo ambavyo kwa sasa wanaume wanavipata kutoka kwa wake zao.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Murufiti wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Chada Salum alisema hayo katika kongamano la wazi la wananchi kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia lililoendeshwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) ambapo alisema kuwa utetezi unaofanywa kwa wanawake umeleta shida kubwa kwa wanaume.

Salum Alisema kuwa historia na vitabu vya dini vinaeleza kuwa mwanaume ndiyo kichwa cha familia lakini kwa sasa wanawake hasa wanaopewa mitaji na serikali na mashirika mbalimbali wamekuwa hawaheshimu waume zao na kufanya mambo ambayo wanajisikia bila kushirikisha waume zao.

“Wanaume kwa sasa tunanyanyasika na wake zetu vya kutosha na ndiyo maana wanaume wanakufa mapema, tunaomba na sisi tupate dawati letu litakalokuwa linawatetea wanaume ili kuepuka vipigo na manyanyaso ambayo wanaume tunapata sasa kutoka kwa wake zetu,”Alisema Chada Salum Mkazi wa Murufiti Kasulu.

Akizungumza katika kongamano hilo Mratibu wa vikundi vya taarifa na maarifa , Flora Ndabaniye kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) alisema kuwa utetezi unaofanywa na taasisi mbalimbali kuwatetea wanawake haulengi kuwakandamiza wanaume badala yake unalenga kuweka uwiano sawa katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye maamuzi mbalimbali.

Flora alisema kuwa historia ilitawaliwa na mfumo dume ambao ulimnyima fursa na nafasi mwanamke katika kushiriki mambo mbalimbali ikiwemo kuibua na kupanga mipango ya familia na kukuta wanawake wakiathirika kwa kiasi kikubwa na maamuzi yaliyokuwa yakifanywa kwenye familia na sehemu za kazi.

“Naomba niwatoe wasiwasi wanaume kwamba mashirika ya utetezi wa mwanamke hayapo kwa ajili ya kuwafanya wanawake kuwa juu ya wanaume au wanawake kuwa na sauti na amri kwa familia zao bali kuweka uwiano wa kushirikiana kwenye kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali,”Alisema Flora kutoka TGNP.

Naye Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya wilaya Kasulu, Zakharia Gabriel alisema kuwa kampeni na uhamasishaji unaofanywa na taasisi mbalimbali na serikali unalenga kuwaweka wanawake karibu katika kushiriki shughuli mbalimbali za kifamilia, shughuli za kiserikali na kuwezesha wanawake kupata elimu kuondoa mfumo dume.

Gabriel alisema kuwa vipo vituo na vikundi mbalimbali vimeundwa kwenye ngazi ya vijiji na kata kwa ajili ya kupinga ukatili wa kijinsia, malezi chanya kwenye jamii lakini ushiriki wa wanaume umekuwa mdogo na wengi wanaona kampeni hizo kama kuwapa kiburi wanawake bila kuwa na uelewa wa mambo hayo.
Mratibu wa vikundi vya taarifa na maarifa , Flora Ndabaniye kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) akizungumza kwenye mdahalo wa wananchi na viongozi wa kijiji cha Murufiti, Nyansha na Kigondo wilayani Kasulu mkoani Kigoma. (Picha na Fadhili Abdallah)
Mratibu wa vikundi vya taarifa na maarifa , Flora Ndabaniye kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) akizungumza kwenye mdahalo wa wananchi na viongozi wa kijiji cha Murufiti, Nyansha na Kigondo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
wananchi wa kijiji cha Murufiti na viongozi wakiwa kwenye kongamano la kupinga ukatili na unyanyasaji kijinsia lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia tanzania (TGNP) lililofanyika kijiji cha Murufiti wiayani Kasulu mkoani Kigoma.


Leokadia Gadjo mkazi wa kijiji cha Murufiti akizungumza kwenye kongamano la kupinga ukatili na unyanyasaji kijinsia lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia tanzania (TGNP) lililofanyika kijiji cha Murufiti wiayani Kasulu mkoani Kigoma
Hekima Meshack Mkazi wa kijiji cha Murufiti akizungumza kwenye kongamano la TGNP kupinga ukatili na unyanyasaji kijinsia.
Viongozi na wananchi wa kijiji cha Murufiti, Nyansha na Kigondo wakiwa kwenye makundi wakijadili mkakati wa kukabili ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwenye jamii za vijiji vyao katika kongamano lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).




Viongozi na wananchi wa kijiji cha Murufiti, Nyansha na Kigondo wakiwa kwenye makundi wakijadili mkakati wa kukabili ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwenye jamii za vijiji vyao katika kongamano lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments