WABUNIFU WATAKIWA KUONGEZA UJUZI KWENYE KAZI ZAO

Zakharia Mfunya mmoja wa wabunifu walioingia fainali ya shindano la ubunifu mkoa Kigoma ambaye alitengeneza mashine rahisi ya kutotoleshea vifaranga. (Picha na Fadhili Abdallah)
Stephano Bika Mshindi wa shindano la ubunifu mkoa Kigoma ambaye alibuni pampu ya kuchotea maji kwenye kisiwa cha wazi.


 Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WITO umetolewa kwa wabunifu mbalimbali mkoani kigoma kuongeza ujuzi kwa vitu wanavyobuni na kutengeneza ili viweze kuleta tija kwenye jamii na kurahisisha utendaji kazi.

Mwalim  Joseph Joachim kutoka cha mafunzo na ufundi  stadi (VETA) Kigoma alisema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya ubunifu ambayo kwa mkoa Kigoma ilitumika kutoa zawadi kwa mshindi wa shindano la ubunifu mkoa Kigoma.

 

Mwalim Joachim alisema kuwa wabunifu hao wanapaswa kuongeza ujuzi ili waweze kufika kwenye hatua nzuri zaidi ili kufanya kazi zao za ubunifu kuweza kutumika mbali zaidi ndani na nje ya nchi.

 

Katika hilo alisema kuwa  ni muhimu kwa wabunifu hao  kuwa na elimu ya ujasiriamali kwani ubunifu huenda sambamba na akili ya utafitaji maarifa zaidi ya kuongeza ubora wa kazi zao za ubunifu lakini kutafuta soko la nje la bidhaa zao za ubunifu.

 

Mchujo huo wa ubunifu ulioratibiwa na shirika la  Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP ) pamoja na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yalikuwa na lengo la kutambua washindi na kutoa zawadi zitakazoendeleza ubunifu wao kwa kununua vifaa vya ufundi vyenye ubora zaidi.

 

Meneja wa SIDO mkoa Kigoma, Gervas Ntahamba alisema kuwa kupatikana kwa wabunifu wa shindano hilo na zawadi zinazotolewa  zinalenga kutambua na kuendeleza vipaji vya wabunifu hao ili kupata mteja utakaowezesha kazi zao za ubunifu kuendelezwa kwa viwango vinavyokubalika ili ubunifu huo usilete madhara.

 

Ntahamba alisema kuwa wabunifu hao wanapaswa kwenda mbali zaidi katika kutengeneza bidhaa zao kwa wingi na kueleza  changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia  ufumbuzi katika suala la utaalam na fedha.

 

Mshindi wa shindano hilo, Stephano Bika kutoka halmashauri ya wilaya ya Kasulu ambaye ametengeneza pump ya maji yenye thamani ya shilingi 520,000 kwaajili ya usalama wa watoto na ulinzi wa mazingira alisema kuwa vifo vya watoto waliokuwa wakitumbukia visimani mara kwa mara ndiyo sababu iliyomfanya kubuni pumpu hiyo  ya maji ili kuwaepusha watoto na hatari hiyo.

 

"Visima vingi vilikuwa wazi, maji yake ni machafu, wakati wa kuchota maji watoto hawana ulinzi kutoka kwa watu wazima, hii pump itawasaidia watoto kutumia wenyewe kuchota maji kwa usalama kwani ni nzuri, rahisi kutumia na haichafui mazingira" amesema Mshindi huyo wa ubunifu

 

Ameongeza kuwa alianza kutumia miti katika ubunifu wake lakini baada ya kupata ushindi wa pesa pamoja na mafunzo ya kuboresha ubunifu wake kutoka shirika la UNDP pamoja na SIDO  aliiboresha pump hiyo ambayo mpaka sasa inatumia chuma.

 

 

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments