SITI AMINA ATUNUKIWA UBALOZI WA UTALII ZANZIBAR

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Simai Mohammed Saidi amemtunuku ubalozi wa utalii katika sanaa na utamaduni Ndg. Amina Omar Juma au Siti Amina katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mkutano wa
 wizara hiyo iliyopo Mnazimoja Zanzibar.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, Mhe. Simai ameeleza kwamba serikali imekua ikiangalia maendeleo ya msanii huyo kulikoenda sambamba na jitihada zake za kuvitangaza visiwa vya Zanzibar kwa kutumia tasnia hii.

 
“ Serikali haijatupa mkuki gizani wakati ikimchagua Siti kuwa Balozi isipokuwa ilifanya utafiti wa kina na kuridhika kwamba ana vigezo via kupatiwa heshima hiyo”,amesema.
 
Bi. Fatma Mabrouk Khamis ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale amempongeza msanii huyo na kusisitiza kwamba heshima aliyopata ni kutokana na jitihada zake katika kufanya kazi pamoja na kutangaza mila,desturi na utamaduni wa wazanzibari.
 
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Khamis Abdallah Said ameeleza kwamba serikali kwa kupitia wizara yake  imekuwa ikifanya kila linalowezekana ili kuwaunga mkono wasanii kutoka Zanzibar ambapo kwa upande wa wizara hiyo wanamtumia msanii Smile the Genius kuwa balozi wao.
  
Kwa upande wake Siti Amina ambae ni kiongozi wa kundi la Siti and the Band wanaotarajiwa kuondoka kesho kuelekea bara ulaya kwa ajili ya  maonesho ya muziki katika nchi za Hispania, Uswizi, Ujerumani, Italy na Austria ameeleza furaha yake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kumpatia heshima hii. 

Ameahidi kutumia matamsha hayo katika kuvitangaza visiwa vya zanzibar pamoja utamaduni kutoka kwa watu wa visiwa hivi.
 
Msanii wa kikaazi kipya kutoka Zanzibar Khalfan Ali Rashid au Fanny ameonesha hisia zake kwa kushukuru serikali kwa kuanza kutambua jitihada za wasanii kutoka Zanzibar.Amesema kwamba amefurahi kuona msanii wa kike kutoka Zanzibar akitapa heshima hiyo kutoka wizara.
 
Siti Amina ni mmoja kati ya waliofaidika na chuo cha muziki cha Dhow Countries Music Academy kilichoanzishwa Mwaka 2002 ambapo imefanikiwa kutengeneza vipaji lukuki vinavyotambulika kimataifa kama vile Nassor Amour(Cholo Ganun wa Rahat Zaman) Mahsin Basalamah( Tara jazz) na Rahma Ameir (Tausi Group.)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments