WAZIRI NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA STAMICO MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI ARUSHA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange kuhusu shughuli wanazofanya leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Waziri Nape Nnauye ametembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Picha na Kadama Malunde 1 blog 
Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange akimwelezea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiipongeza STAMICO kwa shughuli wanazofanya alipotembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani Jijini Arusha yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Kulia ni Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post