Breaking News : WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA..."YANARUSHWA NA MIZIMU"

Mfano wa kifaa cha uganga

***
Katika hali isiyo ya kawaida Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali Mkoani Arusha wametimuliwa kwa kupigwa na mawe ambayo hayajulikani yanapotokea katika kijiji cha Kiwawa kata ya Imbasei wilayani Arumeru Mkoani Arusha.


Inaelezwa kuwa waandishi hao wamekumbwa na masahibu hayo baada ya kufika kwenye eneo hilo kwa lengo la kufuatilia taharuki ya wananchi kupigwa kwa mawe yanayohisiwa kurushwa na Mizimu.


Katika tukio hilo Mwandishi wa GADI TV amejeruhiwa sehemu ya kichwani kwa kupigwa na jiwe huku mwandishi GLOBAL TV akijeruhiwa mkono wake wa kushoto.


Habari kutoka eneo la tukio zinasema nyumba kadhaa zimefanyiwa uharibifu ikiwemo mabati kutobolewa na vioo vya madirisha kuvunjwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments