MBUNGE ATAKA KISUKUMA KIWE LUGHA YA BIASHARA TANZANIA


Mbunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga
**

Mbunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga, amesema Tanzania inabidi ichague lugha kutoka kwenye kabila moja hapa nchini ikiwemo Kisukuma kwa ajili ya kuiweka kwenye system itakayopelekea Wachina ama Wazungu watakapokuja nchini waisomee na itumike katika biashara.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 11, 2022, bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa waangalie mifano kutoka mataifa mengine yanayotumia lugha zao hadi kwenye vyombo vya habari.

"Mimi ni Msukuma lugha yangu mkiipa nafasi mkaweka kwenye system, Kisukuma kikiingia kwenye computer Wachina watakuja kujifunza hapa, hata Wazungu wakija kwenye migodi yetu wakakuta Askari wanazungumza Kisukuma tu hiyo hali itawafanya wakisomee, lazima tukae tufikirie tunawachenga vipi kwenye huu ulimwengu wa kutafuta pesa," amesema Mbunge Maganga.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments