MILIONI 10 ZA BIKO ZATUA KIMARA KWA FUNDI MAJI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2022

MILIONI 10 ZA BIKO ZATUA KIMARA KWA FUNDI MAJI


Balozi wa Biko, Kajala Masanja kushoto, akimkabishi fedha zake mshindi wao wa sh Milioni 10, Ally Kayuni mwenye makazi yake Kimara, jijini Dar es Salaam katikati. Mwingine kulia ni Janeth Msuya, Meneja wa Uhusiano wa CRDB, Tawi la Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga picha wetu.
Mkazi wa Kimara, Ally Kayuni akiwa na shangwe kubwa wakati anakabidhiwa fedha zake sh Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Anayemkabidhi ni Janeth Msuya, Meneja Uhusiano wa Bank ya CRDB, Tawi la Palm Beach, jijini Dar es Salaam. 
Mkazi wa Kimara, Ally Kayuni akiwa na shangwe kubwa wakati anakabidhiwa fedha zake sh Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Anayemkabidhi ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Mkazi wa Kimara, Ally Kayuni akiwa na shangwe 


Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, anayehudumu kama fundi maji wa Mamlaka ya Maji Safi DAWASCO, Tawi la Kimara, Ally Kayuni, amefanikiwa kuibuka na dodo la Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa ya bahati nasibu ya biko, iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kayuni alisema ameshinda baada ya kucheza kwa kuingia www.biko.co.tz na wakati mwingine kutumia mfumo wa namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 jambo lililomfanya atangazwe kama mshindi wa biko..


Alisema Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wamekuwa kuanzia sh 2500 hadi Milioni 5 papo kwa hapo pamoja na droo kubwa za kila Jumapili.


Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages