WAKAZI WA ARUSHA WAOMBA VIONGOZI NCHINI KIFUATA NYAYO ZA HAYATI NYERERE



***************

Na Agness Nyamaru, Arusha.

Katika kuadhimisha miaka100 ya aliyekuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere toka kuzaliwa kwake,baadhi ya wakazi wa mkoa wa Arusha wamesema watamkumbuka kutokana na uzalendo wake wa kuhimarisha umoja na mshikamano nchini.

Wakizungumza na Malunde blog baadhi ya wananchi hao wamesema ni vyema viongozi mbalimbali nchini wakaendelea kuchukua maono yake katika kuyaenzi kwa vitendo pamoja na kuhimarisha uzalendo,umoja na hata kuondoa ukabila.

"Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa kiongozi ambaye aliyetanguliza utaifa wake mbele katika kupambana kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimoja hivyo ni vyema viongozi wanaotuongoza wakafuata nyayo zake,"wamesema nakuongeza kuwa Mwalimu Nyerere ndiye Rais ambaye aliyebakia kwenye taaluma yake ili wananchi wake anaowaongoza wasimuogope.

Kwa upande wake afisa Maonyesho ya Azimio la Arusha,Akonai Bula amesema mchango mkubwa wa aliyekuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Mwalimu Nyerere ulikuwa mkubwa katika taifa ikiwemo Azimio la Arusha katika kuleta usawa kwa binadamu.

Aidha amesema Mwalimu Nyerere alifanya kazi ya kuyaunganisha makabila yote nchini kuwa wamoja hivyo wanakumbuka mchango wake katika azimio la Arusha lililoanzishwa mwaka 1967 na kutangazwa rasmi februari 2 mwaka huo.

"Ukiangalia sera ya azimio la Arusha ni ya ujamaa na kujitemea ambayo hutumika katika maendeleo ya nchi yetu ambapo ilitupitisha katika shughuli mbalimbali ikiwemo kwenye kilimo cha kufa na kupona,"amesema Afisa huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments