SIMBA NA RSB BERKANE ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Na Alex Sonna

SIMBA na RSB Berkane zimetinga kibabe hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi katika mechi zao za mwisho Kundi D.

Simba akicheza uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wameichapa US Gendarmerie mabao 4-0 bao la kwanza likifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 63.

Mabao mawili yamefungwa na Chris Mugalu dakika ya 68 na 78 huku bao la nne akijifunga mlinda mlango wa US Gendarmerie Saidu Hamisu baada ya mpira kurudishiwa na beki wake.

Berkane nao wameifunga ASEC Mimosas bao 1-0 likipatikana dakika ya 28 likifungwa na Chadrack Lukombe kwa Mkwaju wa Penalti

Kwa ushindi huo Timu hizo zimemaliza zikiwa na Pointi 10 kila mmoja huku RSB Berkane wakiongoza wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa nafasi ya tatu ikishikwa na ASEC Mimosas Pointi 9 na US Gendarmerie wakimaliza wa mwisho kwa pointi zao 5.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments