BINADAMU ANAYEDAIWA KUWA MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA


Binadamu anayeaminika kuwa ndiye mzee zaidi duniani Kane Tanaka raia wa Japan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 119.

Tanaka alizaliwa Januari 2, 1903 na inaelezwa kuwa amefariki kutokana na uzee katika hospitali moja katika mji wa Fukuoka, magharibi mwa Japani

Taarifa zinaeleza kuwa mzee huyo alifariki Jumanne Aprili 19 ambapo shirika la utangazaji la serikali ya Japan limethibitisha

Bi Tanaka aliorodhishwa katika kitabu cha Guinness World Records mnamo 2019 kama mtu mzee zaidi aliye hai.

Wakati wa maisha yake, alieleza kuwa alikuwa akipenda chokoleti na vinywaji vitamu
Licha ya umri wake, kwa kawaida aliamka saa kumi na mbili asubuhi na bado alikuwa akijifunza, mara nyingi akisoma masomo mbalimbali kama hesabu

Tanaka alikuwa amepanga kutumia kiti cha magurudumu kushiriki katika mbio za mwenge katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo mwaka 2021, lakini janga la Covid - 19 likazuia ndoto yake hiyo

Katika maisha yake alipata changamoto kadhaa za kiafya ikiwa ni pamoja na kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho na saratani ya utumbo mpana, lakini aliishi 'kwa amani' katika miaka yake ya mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post