WAFARIKI KWA KUFUKIWA NA KIFUSI MACHIMBO YA MAWE KIGAMBONI


Eneo la Machimbo ya Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni Dar es Salaam
**
Watu watatu wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakiwa kwenye shughuli za machimbo ya mawe katika eneo la machimbo ya Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni, Dar es salaam.

Katika ajali hiyo, watu wengine wawili wameokolewa wakiwa hai baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo hayo ya mawe ya Kikikaka, Mjimwema Kigamboni Dar es salaam.

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjimwema, Mohamed Gharib Mohamed amethibitisha na kusema majeruhi wamekimbizwa hospitali. Kwamjibu wa Mwenyekiti wa mtaa huo, ajali hiyo imetokea mapema leo Aprili 3, 2022 saa tatu asubuhi.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post