WANASIASA MASHUHURI UGANDA WAITWA POLISI KUELEZA NAMNA SPIKA WA BUNGE ALIVYOLISHWA SUMU AKAFA



Wanasiasa wa ngazi za juu nchini Uganda wameitwa Polisi ili kuthibitisha madai waliyotoa kwamba, aliyekuwa spika wa bunge la nchi hiyo marehemu Jacob Oulanyah alilishwa sumu jambo lililopelekea kifo chake.

Wanasiasa mashuhuri nchini Uganda akiwemo Robert Kyagulanyi maarufu kama Bob Wine wameitwa Polisi kwa kutoa madai hayo kwamba Jacob Oulanyah amekufa kwa sumu.

Msemaji wa polisi nchini Fred Enanga amesema kuwa walioitwa polisi ni pamoja na Makamu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha NRM Godfrey Kiwanda, Mbunge Santa Okot na Gilbert Olanya

‘’Wanatakiwa watueleze kwa ushahidi jinsi spika alivyolishwa sumu bila kutia shaka yoyote, kwamba nani alimlisha sumu, sumu ilipatikana wapi, na namna yoyote ile inayoonesha marehemu alilishwa sumu.’ Amesema Enanga wakati akizungumza katika makao makuu ya jeshi hilo huko Kampala nchini Uganda.

“Kwa mujibu wa rekodi za afya tulizonazo, hakukua na sumu kwenye damu yake . sasa tunataka wao waje kututhibitishia’’

Siku ya jana, Bw. Kyagulanyi maarufu kama Bob Wine ambaye pia alihudhuria maziko aliitaka serikali kufanya uchunguzi wa kutosha juu ya madai ya sumu iliyosababisha kifo cha spika huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments