MEYA WA MANISPAA YA MOSHI ANG'OLEWA


Madiwani wa Manispaa ya Moshi wamepiga kura ya kumuondoa meya wa wa manispaa hiyo Juma Raibu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Kura 18 zimemuondoa madarakani Meya huyo kutokana na tuhuma nne zinazomkabili ikiwemo tuhuma za rushwa katika vibali vya ujenzi majengo katika halmashauri ya manispaa hiyo

Tuhuma nyingine zinazomkabili ni matumizi mabaya ya madaraka pamoja na mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu dhidi ya madiwani wenzake.

Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Rashid Gembe amesema kura 28 zilizopigwa na madiwani hao kura 18 zilikuwa za ndiyo na kura 10 zikisema hapana jambo ambalo lilihitimishwa kwa mujibu wa kanuni na Meya huyo kuong’olewa madarakani

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post