NSSF YATWAA TUZO YA UTOAJI ELIMU BORA KATIKA KILELE CHA SIKU YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akipokea Tuzo ya kundi la watoa Elimu bora kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Dkt. Profesa Joyce Ndalichako katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma.

Tuzo hiyo ni kielelezo tosha kuwa NSSF ilifanikiwa kuwafikia baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya jirani kwa ufanisi mkubwa.

 Ahadi ya NSSF ni kuendelea kutumia mikakati mbalimbali kutoa elimu kwa faida ya wanachama kutoka Sekta Binafsi na Sekta Isiyo Rasmi Nchi mzima, ambapo katika Maonesho ya OSHA NSSF inatoa elimu ya hifadhi ya jamii, uelewa kuhusu mifumo na kupokea kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akitoa maelezo kwa Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Profesa Joyce Ndalichako, kuhusu kazi zinazofanywa na NSSF katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea Mkoani Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NSSF katika kilele cha Maonesho ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akipata maelezo katika banda la WCF kuhusu huduma zinazotolewa na WCF
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akipata maelezo kutoka kwa Grace Michael, Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuhusu huduma wanazozitoa katika maonesho ya OSHA wakati alipotembelea banda la NHIF


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments