WAZIRI GWAJIMA ATEMBELEA KABURI LA MTOTO ALIYEUAWA KWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO NA BIBI YAKE...AZUNGUMZA NA WANANCHI WA LYABUKANDE

 


Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, (wa tano kutoka kulia) akiwa katika kaburi alilozikwa mtoto Joseph Juma (4) ambaye alidaiwa kuuawa na bibi yake Tatu Moshi kwa kipigo na kumwagiwa maji ya moto katika kijiji cha Lyabukande wilayani Shinyanga.

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, akimjulia hali mtoto Limi Lameck mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba, katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga ambaye alipata majeraha na kunusirika kifo kutoka kwa bibi yao Tatu Moshi, ambaye aliwapiga na kaka yake kufariki dunia.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZIRI wa maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, ametembelea kwenye kaburi alilozikwa mtoto Joseph Juma (4) ambaye alidaiwa kuuawa na Bibi yake Tatu Moshi (45) mkazi wa kijiji cha Lyabukande wilayani Shinyanga kwa kipigo na kumwagiwa maji ya moto.

Waziri Gwajima ametembelea leo kaburi hilo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, huku akifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Lyabukande kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Alisema ameamua kufanya ziara mkoani Shinyanga, mara baada ya kusikia tukio hilo la mauaji ya mtoto huyo, pamoja na mdogo wake Limi Lameck mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi Saba, kujeruhiwa kwa kipigo na bibi yao, ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufani mkoani humo ili kukemea vitendo hivyo vya ukatili.

"Baada ya kusikia tukio hili la mauaji ya mtoto Joseph Juma, pamoja na mdogo wake Liimmy Lameck ambaye yeye alinusurika kifo kutokana na vipigo vya bibi yao limenigusa na kuamua kufanya ziara hapa Shinyanga pamoja na kumuoa Bibi huyo na kutembelea kaburi ambalo amezikwa mtoto huyo," alisema Gwajima.

"Nalaani sana matukio haya ya ukatili, sababu hatuwezi kuwa na maendeleo kama kila kukicha unasikia mauaji, nataka ifike mwisho tusisikie tena mauaji dhidi ya watoto," aliongeza.

Aidha, aliitaka pia jamii wanapoona au kusikia mtoto wa jirani anafanyiwa vitendo vya ukatili, watoe taarifa mapema ili kudhibiti matukio hayo ambayo yamekuwa yakileta madhara na hata kusababisha mauaji.

Alisema Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho (2019) ina kataza mzazi kumuudhibu mtoto na kumsababishia madhara kwenye mwili wake, na kuwataka wazazi kuacha kutoa adhabu kali kwa watoto wao na hata kuwasababishia umauti.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, alisema katika uchunguzi walioufanya walibaini pia watoto hao, walikuwa wakifungiwa ndani kila siku, wakati bibi na mama yao walipokuwa wakienda kutafuta riziki, lakini wana jamii walikuwa hawatoi taarifa na kufumbia macho vitendo hivyo.

Aidha, alisema Serikali mkoani humo wanafanya utaratibu wa kutafuta mlezi ambaye atamlea mtoto huyo kwa muda, wakati mama yake akiendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi akiwa na bibi yao anaye tuhumiwa kusababisha mauaji, na kubainisha kuwa akikosekana mlezi ataendelea kuwa chini ya Serikali.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, aliwataka pia viongozi wa dini wakemee vitendo hivyo vya ukatili, pamoja na viongozi wa Sungusungu kuwa mstari wa mbele kupinga matukio hayo.

Kwa upande wake Ofisa maendeleo ya jamii mkoani Shinyanga Tedson Ngwale ,alitaja takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto mkoani humo, kuwa kuanzia mwaka 2021 hadi March 2022, kuwa kesi zilizolipotiwa 3,288, watoto wa kike 2625 na wakiume 663.

Tukio hilo la mauaji ya mtoto huyo Joseph Juma( 4) pamoja na kujeruhiwa mdogo wake kwa kipigo na bibi yao, lilitokea April 18 mwaka huu majira ya saa 11 alfajiri, katika kijiji cha Lyabukande wilayani Shinyanga, kwa madai ya kujisaidia hovyo na Bibi huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga pamoja na mama yao Helena Nicolaus.


Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, akizungumza na wananchi wa Lyabukande wilayani Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara na kukemea vitendo vya ukatili kuendelea ndani ya jamii.

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, akiendelea kuzungumza na wananchi wa Lyabukande kwenye mkutano wa hadhara.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akielezea hali ya matukio ya ukatili mkoani Shinyanga.

Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, akitoa taarifa ya matukio ya ukatili mkoani humo.

Mjumbe wa baraza la Nacongo Mussa Ngangala akizungumza kwenye mkutano huo, na kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake mkoani Shinyanga.

Wananchi wa Lyabukande wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Mwananchi Noah Mhango akishukuru wananchi kupewa elimu ya kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo walikuwa hawana na kuomba iwe inatolewa mara kwa mara.

Mwananchi Sabina Fumbuka, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara na kushukuru kupewa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima (katikati) akiingia Hospital ya Rufani mkoani Shinyanga, kumjulia hali mtoto Limi Lameck mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba, ambaye alinusurika kifo baada ya kupigwa na bibi yake Tatu Moshi na kumsababishia majeraha mwilini, huku kaka yake akipoteza maisha kwa kipigo na kumwagiwa maji ya moto. (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk Yudas Ndungile.

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, akimjulia hali mtoto Limi Lameck mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba, katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga ambaye alipata majeraha na kunusirika kifo kutoka kwa bibi yao Tatu Moshi, ambaye aliwapiga na kaka yake kufariki dunia.

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, (kushoto) akisalimia na Katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omari (kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati) alipowasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya siku mbili.

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) alipowasili mkoani Shinyanga.

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima, (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wapiga picha ya pamoja na watoto kwenye mkutano wa hadhara Lyabukande wilayani Shinyanga na kuonyesha jamii kuwapenda watoto na siyo kuwafanyia vitendo vya ukatili.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments