WATOTO 637,720 CHINI YA MIAKA MITANO KUPEWA CHANJO YA MATONE YA POLIO KAGERA


Msimamizi wa Taifa Chanjo ya Polio Mkoa wa Kagera Regina Joseph akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya Afya ya msingi Mkoa kuhusu kampeni ya utoaji wa matone ya Chanjo ya Polio Mkoani Kagera
Msimamizi wa Huduma za Chanjo Kagera Zablon Segeru akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya Afya ya msingi Mkoa kuhusu kampeni ya utoaji wa matone ya Chanjo ya Polio Mkoani Kagera
Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa Kagera Dkt. Issessandaa Taniki aliyekaa ni Mwenyekiti wa Kikao cha kamati ya Afya ya msingi Mkoa kuhusu kampeni ya utoaji wa matone ya Chanjo ya Polio Mkoani Kagera Khalifa Shemahonge
Wajumbe wa Kikao cha kamati ya Afya ya msingi Mkoa kuhusu kampeni ya utoaji wa matone ya Chanjo ya Polio Mkoani Kagera
Wajumbe wa Kikao cha kamati ya Afya ya msingi Mkoa kuhusu kampeni ya utoaji wa matone ya Chanjo ya Polio Mkoani Kagera

**

Na Mbuke Shilagi Kagera.


Watoto 637,720 wenye umri chini ya miaka mitano wanatarajiwa kupata chanjo ya matone ya Polio mkoani Kagera.

Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Kagera Zablon Segeru wakati wa kikao cha kamati ya Afya ya msingi Mkoa kuhusu Kampeni ya utoaji wa chanjo ya Polio mkoani humo kilichohudhuriwa na viongozi wa idara mbalimbali kwa lengo la kuweka mipango ya kufanikisha zoezi hilo.


Segeru amesema kuwa watoto hao wanatakiwa kupata chanjo, ili kuwakinga na kirusi cha polio kilichogundulika nchini Malawi.


Amesema kuwa watoto wote mkoani humo wanatakiwa kufikiwa na chanjo hiyo ili kuhakikisha wanawakinga na ugonjwa huo kutokana na mwingilio ambao unasababishwa na mkoa kupakana na nchi nyingi.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo itakuwa na timu ambayo itazunguka nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuwafikia walengwa wote ambao ni watoto wenye umri sifuri mpaka miaka mitano.


Msimamizi huyo wa chanjo amesema kuwa ugonjwa wa polio ni hatari maana husababisha kupooza na kusababisha mhusika kupata ulemavu wa kudumu.

Kwa upande wake Afisa kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Regina Richard amesema kuwa chanjo hiyo ndiyo ile ile ambayo wazazi huwapeleka watoto wao kupata mara baada ya kujifungua na kuwa haina madhara yoyote kwa mtoto isipokuwa kumlinda.

Ameongeza kuwa mbali na chanjo kupita nyumba kwa nyumba hata katika mikusanyiko itakuwepo timu ambayo itapita kila kona kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo na kwamba wataweka alama kwa watoto watakaochanjwa pamoja na nyumba, ili kutambua waliopata na ambao bado.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments