MKOA WA MANYARA WASUASUA UWEKAJI WA VIBAO ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI


Na Beatrice Mosses -MANYARA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis ametoa agizo kwa mkoa wa Manyara mpaka kufikia tarehe 05.05.2022 halmashauri zote mkoani humo ziwe zimeshakamilisha zoezi la uwekwaji wa vibao na  namba kwenye anwani za makazi.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya Halmashauri zote za mkoa wa Manyara kusuasua katika zoezi la anuani za makazi ambapo ripoti ya zoezi la anuani za makazi nchini inawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri  ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu ifikapo tarehe 10 mwezi wa 05 mwaka huu.


"Leo ni tarehe 29 mwezi wa nne,  ripoti ya mwisho itawasilishwa tarehe 10 ya mwezi wa tano mimi mwenyewe binafsi nisingependa kuona ripoti inawasilishwa halafu nyie bado mko chini,  haitakuwa nzuri,  tutatuma timu ya wakaguzi kuna kukagua utekelezaji wa tuliyokubaliana kabla ya tarehe 10  ili ikitoka ile ripoti ya mwisho Manyara iwe imetoka kwenye ile Red line.


 "Mhe. RAS nakuachia wewe lakini hapa tunakubaliana hadi kufika tarehe tano mwezi wa tano muwe mmeshakamilisha ili ikifika tarehe sita na saba tutatuma timu kuja kukagua mpaka kule chini,  tutaangalia nyumba pamoja na mitaa,  tarehe nane tukirudi ofisini tunaandika ripoti ili na wao wapende kwenye ile redline",  amesema Khamis.


Nao baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali mkoani Manyara wanasema changamoto zinazokwamisha zoezi la anuani za makazi ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi na gharama kubwa za vibao na nguzo ni moja ya sababu iliyosababisha zoezi hilo kusuasua


"Nguzo ni 18 zilizosimikwa halafu 12 ni za taasisi  ni kama nguzo 30 na katika makazi ni vibao vichache sana kama vibao 45 tu kati ya vibao 95412,  kitu ambacho ni changamoto ni gharama kubwa ya nguzo kwa sababu uliangalia kwenye vile vibao 95412 gharama inakuwa ni kubwa na jumla ya hizo gharana ukiangalia inakuwa ni karibu mil. 961 kwa hiyo ni zoezi ambalo tunaendelea kuhamasisha wadau na makampuni mbalimbali waweze kutusaidia", amesema Anna Mbogo,  mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbulu Mjini Yefred Myenzi amesema kwamba changamoto ya uelewa wa jamii wanapoenda kufanya zoezi hili jamii inakuwa haitoi ushirikiano na wamiulizwa kwanini wanajibu basi tu sitaki tu kutoa taarifa.


  "Kuna wale ambao hawataki tu kutoa taarifa,  na tumekutana na situation kama hizo  mimi sitaki sitaki tu kutoa taarifa na tumewakuta wako wengi tu wa hivyo na Mbulu ni moja ya maeneo ambayo mwitikio wa jamii kwa masuala kama haya kuwa ni mgumu na ni jamii yenye mila na desturi ambazo ni ngumu kidogo kwa hiyo inabidi utumie muda mwingi kuhamasisha na kuelimisha angalau tuende pamoja",amesema Myenzi.

  

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments