VIKUNDI 271 VYANUFAIKA NA TEKNOLOJIA YA UZALISHAJI WA MAFUTA YA PARACHICHI

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Avomeru Group Jesse Oljange akionesha waandishi wa habari mashine za uzalishaji wa mafuta ya parachichi.

Na Rose Jackson, Arusha
Vikundi 271 vya Wakulima vimenufaika na teknolojia ya uzalishaji wa mafuta ya parachichi ambapo kupitia uzalishaji huo vikundi hivyo vimeuza mafuta na kuona faida yake.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Avomeru Group inayozalisha mafuta kutoka matunda ya parachichi Jesse Oljange wakati akizungumza na waandishi wa habari waliopatiwa  mafunzo na COSTECH mara baada ya kutembelea kampuni hiyo kwa lengo la kujifunza habari za matokeo ya utafiti wa sayansi.

Amesema kuwa toka mwaka 2017 walivy anza kutengeneza vikundi ,vikundi 271 vimenufaika na teknolojia ya uzalishaji wa mafuta ya parachichi ambapo wameshauza mafuta na kupata faida.

"Kwa sasa tuna jumla ya vikundi 487 kule vijijini lakini ambao wamefikiwa na teknolojia hii ya uzalishaji ni vikundi 271 hawa tayari wameshaona faida za teknolojia hii lakini wapo jumla ya Wakulima zaidi ya elfu kumi na tisa wanauhitaji wa kufikiwa na teknolojia hiyo",alisisitiza Oljange.

Akielezea upande wake soko amesema kuwa asilimia kubwa wanauza mafuta kwa jumla ambapo wamekuwa wakiingiia makubaliano na wateja ambao wanasubiri mzigo kwa kuwa uhitaji ni mkubwa.

Amesema mafuta wanayozalisha ni mafuta ghafi ambayo yana uwanja mpana kwenye soko kwani ni rahisi kuuza kwenye kampuni za vipodozi.

Aidha ameeleza namna ambavyo COSTECH ilivyowezesha kampuni hiyo kufikia ndoto yake amesema kuwa ilimwezesha kupata mkopo wa fedha ambazo aliweza kufunga mashine na kuwafuata wakulima vijijini na hatimaye kuendelea kupanuka mara baada ya COSTECH kumwamini.

"Naishukuru COSTECH maana iliweza kuniamini na kunipa mkopo ambao niliweza kuanza kwa kufunga mashine za uzalishaji na kuweza kuwafikia Wakulima kule vijijini kuwapatia mafundi hivyo waliniamini na kuweza kunitia moyo kumbe naweza maana mara ya kwanza walinipa milioni 14 ambazo zilinijengea uwezo na ujasiri",aliongeza .

Amedai kuwa lengo lao ni kuongeza thamani kwenye zao la parachichi kwa wakulima ili waweze kupata faida kwa asilimia mia moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post