LAAC YAKAGUA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA MAGU


Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imekagua ujenzi wa ofisi ya Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi, Kaimu Mwenyekiti Mhe. Aloyce Akwezi (Mb) ameipongeza Halmashauri kwa jengo imara litakalowafikishia huduma wananchi kwa karibu.

Pia amewataka TAMISEMI kuhakikisha wanaleta fedha zilizobaki ili kuweza kukamilisha mradi uliochukua zaidi ya miaka kumi.

Naye Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Dkt. Festo Dugange amewahakikishia kamati kuwa amepokea maelekezo ya kuleta fedha kwa mradi huo uliogharimu takribani bil 7 na utaisha kwa wakati.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Ngusa Samike amepokea salamu za pongezi na kusema ushirikiano wa viongozi wa Mkoa umeweza kuleta mafanikio.

 Kukosekana kwa migogoro ndio kumeleta mafanikio makubwa Halmashauri ya Magu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments