MKUU WA MAJESHI AWASAMEHE VIJANA WA JKT 853 WALIOFUKUZWA KAMBINI, AAMURU WARUDI MAKAMBINI



Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo
**

Na Samir Salum 


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa Vijana  853 waliofukuzwa katika kambi za JKT April 12, 2021 kutokana na makosa ya kinidhamu.


Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Machi 05, 2022 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda amesema kuwa CDF Mabeyo  ameamuru Vijana hao wote warejeshwe katika Makambi ya Kujenga Taifa tayari kwa kuanza mafunzo yao mara moja.


Amesema kuwa Mnamo April 12,2021  Jumla ya Vijana wa Kitanzania 854 ambao walikuwa wanaendeea na mafunzo ya kujitolea kwenye Makambi ya JKT, walifukuzwa na kuondolewa makambini na kurejeshwa majumbani mwao kutokana na sababu za kimakosa ya kinidhamu.


"JWTZ imepokea na ina taarifa Kijana mmoja kati ya wale Vijana 854 amefariki na walio hai ni Vijana 853" amesema 


Luteni Kanali Ilonda ameeleza kuwa Msamaha ambao Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo ameutoa kwa Vijana hao umetokana baada ya JWTZ kufanya uchunguzi wa kina na utafiti na kujiridhisha na kuonesha kuwa vitendo hivyo vya ukiukwaji wa taratibu za kinidhamu walivyifanya ni kwasababu ya utoto.


"wengi wao walifanya hivyo kwa kutojitambua, kurubuniwa na wengine walifanya kwa kufuata mkumbo" amesema Luteni Kanali Ilonda

Aidha, Luten Kanali Ilonda ameongeza kuwa kuna baadhi ya Watanzania walioshiriki kuwarubuni Vijana hao na kutoa wito wa kutofanya vitendo hivyo


"tuache Vijana wapate mafunzo yao ya stadi za maisha ili waje kulitumikia Taifa lao kwa moyo mmoja" Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ)

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post