DKT. JAFO ATEMBELEA BANDA LA TBS KWENYE MAONESHO YA WAJASIRIMALI WANAWAKE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimueleza jambo Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Masoko TBS,Bi. Gladness Kaseka mara baada ya kutembelea banda la TBS katika Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya maafisa viwangoo wa TBS mara baada ya kutembelea banda hilo leo katika Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Amiti Msanjila akikagua baadhi ya bihaa za wajasiriamali katika Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) ameipongeza TBS kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha bidhaa za wajasiriamali zinapata leseni ya kutumia alama ya ubora na hatimaye kupata masoko ndani na nje ya nchi.

Waziri Jafo ametoa pongezi hizo leo mara baada ya kutembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, Waziri Jafo amesema uwepo wa TBS katika maonesho hayo kutawarahisisha wajasiriamali wanawake kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu Viwango .

Amesema suala la viwango ni muhimu hasa katika masuala ya biashara, hivyo kupitia maonesho hayo yatawajengea uelewa mkubwa wajasiriamali namna watakavyotumia viwango kwenye biashara zao na kuhakikisha biashara zao zinakidhi viwango.

Kwa upande wake Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Amiti Msanjila amesema wameendelea kuwapa msaada wajasiriamali namna ya kuweza kupata alama ya ubora kwenye bidhaa zao, usajili wa majengo ya vipodozi na chakula.

Amesema takribani wajasiriamali 500 wameshapewa nembo ya ubora kwenye bidhaa zao bure mara baada ya kufuata taratibu zinazotakiwa.

"Ukiwa na alama ya ubora kwenye bidhaa zako itakusaidia kukuza biashara yako kwa kuaminika kwenye soko pia anaweza akasafirisha bidhaa yake kupeleka nchi yoyote Duniani". Amesema.

Aidha amewataka wajasiriamali kuhakikisha bidhaa zao zimekaguliwa na TBS na zinakidhi viwwango vinavyotakiwa ili kuweza kumlinda mlaji wa bidhaa hiyo pasipo kumletea madhara

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments