TEMDO YAFANIKIWA KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA UAGIZWAJI WA VIFAA TIBA KUTOKA NJE YA NCHI

Mkurugenzi wa TEMDO Mhandisi Fredrick Kahimba akiwaelezea waandishi wa habari Teknolojia ambazo zimebuniwa na taasisi hiyo ikiwemo vitendea kazi vya hospitalini.

Na Rose Jackson,Arusha

Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) imetengeneza vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia kwenye hospitali ili kupunguza uagizwaji wa vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Temdo Mhandisi Fredrick Kahimba wakati akitoa taarifa za utafiti  kwa waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) waliofika katika taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza habari za matokeo ya utafiti.

Mhandisi Kahimba amesema kuwa wameweza kubuni na kutengeneza vifaa tiba hivyo kwani kwa muda mrefu serikali imekuwa ikiagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

"Vile vituo vya afya vilivyojengwa nchi nzima kwa sasa kuna uhakika wa kupata vifaa tiba vyake hapa hapa TEMDO badala ya kuagiza tena kutoka nje ya nchi", aliongeza mhandisi Kahimba.

Ameongeza kuwa mbali na kutengeneza vifaa tiba hivyo taasisi hiyo imeweza kutengeneza mashine mbalimbali ambazo zina uwezo wa kuendesha viwanda vikubwa na vya kati ikiwemo mashine za kukamulia Alizeti pamoja na nyinginezo.

Amedai kuwa tasisi hiyo pia ina uwezo wa kupokea mawazo ya ubunifu wa mashine kutoka kwa wadau mbali mbali na wahandisi wabunifu wa TEMDO wakaweza kutengeneza teknolojia ambayo ina uwezo wa kusaidia jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi hao Abraham Gwandu aliishukuru COSTECH kwa mafunzo ya utafiti wa sayansi ambapo wameahulidi kuyatumia katika kuisadia jamii kujua matokeo ya tafiti zinazofanywa na wabunifu na watafiti mbali mbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments