WATU WANNE WAFARIKI, 13 HOI KWA KUNYWA POMBE


Raia wakiwa wamekusanyika eneo la tukio

**

Watu wanne wamefariki huku wengine 13 wakilazwa hospitali baada ya kunywa pombe haramu.

Tukio hilo limetokea Jumanne, Machi 22,2022 walipoteza maisha yao baada ya kunywa pombe haramu katika kijiji cha Canaan katika wadi ya Kamukuywa, eneo bunge la Kimilili nchini Kenya.

Waathiriwa waliripotiwa kulalamikia kuumwa na tumbo na uchovu wa jumla wa mwili baada ya kunywa pombe hiyo inayojulikana kama changaa. 

Walioshuhudia kisa hicho wanadai wanawake hao watatu na mwanaume mmoja walikunywa kinywaji hicho, kisha wakakimbizwa katika zahanati iliyoko karibu.

Mmoja wa wanawake hao alikuwa muuzaji wa pombe hiyo.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kimilili, Muita Marwa, alisema wengine kadhaa walianza kuugua.

Alisema kumi na watatu walilazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kimilili chini ya hali mbaya.

 Akihutubia wanahabari kutoka nyumbani kwake, Richard Kasayi, mwenyeji wa eneo hilo, alisema walikuwa wakishuku mchezo mchafu katika kile kilichosababisha vifo vya watu hao wanne lakini mamlaka inachunguza.

 Kasayi alisema alipokea habari kwamba kuna mtu aliweka sumu kwenye kinywaji hicho na kusababisha vifo vya watu hao wanne, akiwemo mgema.

 "Inasemekana ni kama kuna mtu inakaa aliweka sumu kwa hiyo pombe. Ndiposa tunajaribu kuangazia hii sumu ilipatikana aje. Pia inachanganya ya kuamba walioathirika walikunya hii pombe mahali tofauti. Tunashindwa kujua ni nyumba gani. Mimi nita waomba wananchi wawe watulivu tuachie serikali kazi yake," alidokeza Kasayi.

Polisi wanawatafuta wanaosemekana kuuza pombe hiyo inayodaiwa kutiwa sumu.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments