Tazama Picha : SHEREHE ZA WANAWAKE SHINYANGA 'WOMEN'S DAY OUT' 2022

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na wanakikundi cha Women For Change.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikata keki kwenye sherehe hiyo ya wanawake Women's day out, ambayo imeandaliwa na kikundi cha wanawake Women For Change

Na Marco Maduhu, Shinyanga

SHEREHE ya wanawake Women's day Out, ambayo imeandaliwa na kikundi cha wanawake Women For Change Manispaa ya Shinyanga, imefana kwa kukutanisha wanawake na kupatiwa mafundisho ya mada mbalimbali za kuwajenga kifamilia na kujikwamua kiuchumi.

Sherehe hizo zimefanyika Machi 12,2022 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na chama, ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa Sherehe hizo, Mboneko amewataka wanawake wa Shinyanga, wachangamkie fursa ambazo zipo ndani ya Shinyanga ili ziwakwamue kiuchumi.

Alisema Manispaa ya Shinyanga ina fursa nyingi ambazo wanawake wanaweza kuzitumia na kuinuka kiuchumi, ikiwamo kumiliki viwanja hasa kwenye maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji.

"Najua wanawake wa Shinyanga ni wachakalikaji, hivyo nawasihi mchangamkie fursa za kiuchumi ambazo zipo hapa Shinyanga, ambapo katika Manispaa ya Shinyanga kuna maeneo ambayo tunapima viwanja, pia kuna ujenzi wa kiwanja cha ndege, stendi kuu ya mabasi changamkieni hizo fursa kuwekeza Mahotel," alisema Mboneko.

"Uzuri sasa hivi kupata hati ya kiwanja ni hapa hapa Shinyanga, na siyo kwenda Simiyu kama zamani, na mtakapopata changamoto zozote msisite kusema ili tuitatue," aliongeza.

Katika hatua nyingine, aliwataka wanawake washikamane katika masuala ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi yao, na kuwasaidia wenzao ambao hufanyiwa vitendo hivyo, ili kuwafuta machozi na kusonga pamoja katika gurudumu la maendeleo.

Aidha, Mboneko alikipongeza pia kikundi hicho cha wanawake Women For Change, kwa kurudisha fadhila ndani ya jamii kwa kile ambacho wanakipata, na kutoa misaada mbalimbali ikiwamo ya Madawati na hata kukarabati bweni la wanafunzi wenye uhitaji katika kituo cha malezi buhangija.

Kwa upande wa utoaji mada mbalimbali kwenye sherehe hiyo ya wanawake, ambapo mtoa mada wa kwanza Tumsifu Matutu, mtaalam wa malezi na mahusiano, akitoa mada hiyo ya malezi, aliwasihi wanawake kuwa wanapodai masuala ya usawa wa kijinsia wasiache majukumu yao mengine kama mama ikiwamo malezi ya watoto na kunyonyesha.

Alisema mwanamke ndiyo mlinzi wa kwanza wa familia na ndiye ana mwandaa mtoto wake atakuwa nani badae kutokana na jinsi atakavyo mlea, na kuwahisi wanawake wasisahau majukumu yao ndani ya familia.

Aliwasisitiza pia wanawake wawe wanatenga muda wa kukaa na watoto wao na kusikiliza changamoto zao na kuzitatua na siyo kushinda wakichezea simu, ili kuendelea kuwajenga watoto kimaadili, kiakili na kutimiza ndoto zao.

Mtoa mada wa pili Mwakanyamale Mwakatundu ambaye mbobezi masuala ya uchumi, naye aliwasihi wanawake wa Shinyanga ili wapate kufanikiwa kimaisha lazima waanze na utatuzi wa matatizo ,huku akitoa mbeleko tatu za kiuchumi ambazo ni Mtaji, Ardhi, na watu.

Alifafanua mbeleko hizo kuwa mtaji alimaanisha akili, yani mwanamke anapaswa na akili ya kubaini fursa ya eneo lake na kuitumia vizuri kujikwamua kiuchumi, huku akitolea mfano wa mwanamke ambaye alitumia fursa ya kuuza makongoro baada ya kuona eneo analokaa kuna mafundi gereji ambao huwa wanamka na pombe kichwani ikabidi atumie fursa hiyo na akakua kiuchumi.

Akizungumzia ardhi, alisema anamaanisha kuwa mwanamke lazima awe na ardhi yake mwenyewe ambayo ana imiliki kwa jina lake na siyo ya familia, na kwa upande wa mbeleko ya tatu ya watu, alimanisha wapunguze maadui na kuongeza marafiki ndipo watasonga mbele kimaendeleo.

Mtoa Mada wa tatu mchungaji Faustin Kamugisha, yeye alitoa mada ya mwanamke usiyapoteze machozi yako machozi ni Tiba, na kuwaasa wanawake kuwa jambo baya katika maisha ni kukata tamaa, na kuwasihi wasijione dhaifu bali wafute machozi waamke na kupambana kimaisha.

Nao baadhi ya wanawake ambao walihudhuria Sherehe hiyo, kwa nyakati tofauti walisema wamejifunza mambo mengi ambayo yatawasaidia katika maisha yao.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha wanawake Women's For Change Ansila Benedict, alisema seherehe hizo zitaendelea kufanyika kila mwaka, kwa kuleta watoa mada tofauti ambao watawajenga wanawake katika familia zao na kuwakuza kiuchumi.

Pia aliwapongeza wadhamini waliowaunga mkono na kufanikisha sherehe hiyo ambao ni Winterfell, Little Treasures School, Hilbat Pre and primary School, Msilikare Micro Credit, Shybest, Beirbamas Travel Agent, Jambo, Mama Diariesm VRK Traders, Diamon Royal Hotel, UTT Amis, Bwihas, Fk Grand kitchen,Lulekia Company, BM Investment, Jeminaely home Shoping Center.

Wengine ni Mama Kweka House of Tiles, Hahosa Stationary, St Joseph Collenge, Sheer Bliss School, Vai Saloon, Mama Love Decoration, Ommy Fashion, Bonga Security, Ekisha Printing, Brother hood, Kom School, Shuwasa, Lope Catering, Dewin Cake pamoja na Hope Extended Secondary Secondary.

Kauli mbiu yao ya mwaka huu kwenye sherehe hiyo ya wanawake inasema WOMEN’S DAY OUT, “Amka, Futa chozi, Pambana, 2022 twende pamoja”.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Sherehe hiyo ya wanawake Womens day Out.
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake Women For Change Ansila Benedict akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Mwenyekiti wa Sherehe ya wanawake Faustina Kifambe akizungumza sherehe hiyo.
 
 MC Mama Sabuni akisherehesha sherehe hiyo.
Tumsifu Matutu ambaye ni mtaalam wa malezi na mahusiano, akitoa mada ya malezi kwenye sherehe hiyo.
Tumsifu Matutu ambaye ni mtaalam wa malezi na mahusiano, akiendelea kutoa mada ya malezi kwenye sherehe hiyo.
Mtaalam wa uchumi Mwakanyamale Mwakatundu, akitoa mada kwenye sherehe hiyo.
Mchungaji Faustin Kamugisha kutoka Bukoba, akitoa mada kwenye sherehe hiyo.
Wanawake wakiwa kwenye sherehe ya 'Women's day Out' iliyoandaliwa na kikundi cha Women For Change.

Wanawake wakiwa kwenye sherehe ya 'Women's day Out' iliyoandaliwa na kikundi cha Women For Change.Wanawake wakiwa kwenye sherehe ya 'Women's day Out' iliyoandaliwa na kikundi cha Women For Change.Wanawake wakiwa kwenye sherehe ya 'Women's day Out' iliyoandaliwa na kikundi cha Women For Change.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikata keki kwenye sherehe hiyo ya wanawake.
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake Women For Change Ansila Benedict,(kulia) akimlisha keki Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwenye sherehe hiyo.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akimlisha keki Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake Women For Change Ansila Benedict kwenye sherehe hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto)akimlisha keki Mwenyekiti wa Sherehe hiyo Faustina Kifambe ambaye pia ni Mhasibu wa kikundi cha wanawake Women For Change.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akitoa vyeti vya pongezi kwa wadhamini ambao walikiunga mkono kikundi cha wanawake Women For Change ili kufanikisha sherehe hiyo ya wanawake Women's day Out.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea kutoa vyeti vya pongezi kwa wadhamini.
Zoezi la utoaji vyeti vya pongezi kwa wadhamini likiendelea.

Kikundi cha wanawake Women For Change, wakitoa zawadi ya mkufu wa shingoni kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Wanawake wa kikundi cha Women For Change, wakiwa kwenye sherehe ya wanawake ambao wao ndiyo wameiandaa.
Msanii wa Singeli Msagasumu akitoa burudani kwenye sherehe hiyo.
Msagasumu akiendelea kutoa burudani.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati) akiingia ukumbini kwenye sherehe hiyo ya wanawake, (kushoto) ni mwenyekiti wa kikundi cha wanawake Womens For Change Ansila Benedict na (kulia) ni Mwenyekiti wa sherehe hiyo Faustina Kivambe.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (wapili kushoto) akipiga picha ya pamoja na watoa mada kwenye sherehe hiyo, (kushoto) ni Mtaalam wa malezi na mahusiano Tumsifu Matutu, na (kulia) ni Mchungaji Faustin Kamugisha, akifuatiwa na Mchumi Mwakanyamale Mwakatundu.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na watoa mada kwenye sherehe hiyo, na baadhi ya viongozi wa kikundi cha Women Fof Change, akiwamo Mwenyekiti wa kikundi hicho Ansila Benedict (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa sherehe hiyo Faustina Kivambe na pia ni Mhasibu wa kikundi hicho.

CHANZO SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post