MWANAMKE KIONGOZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

MWANAMKE  KIONGOZI 

1.     Ninaanza kwa Imani, kumshukuru Mwenyezi

Kwa rehema na amani,upendo tunauenzi

Turudishe shukrani, kwa yake mema mapenzi

Mshikamano na Amani, tuendelee kuvienzi

 

2.     Nampongeza wa sita   Rais  kashikilia

Kamwe hakusitasita,  uongozi shikilia

Miongoni mwa  nchi sita, mwanamke kashikilia

Mshikamano na Amani, tuendelee kuvienzi

 

3.     Kwa yake kauli mbiu,kazi inaendelea

Usafiri,afya elimu,mapambano yanaendelea

Umeme,maji ,nidhamu,yote yanaendelea

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi 

 

4.     Mwanamke ni  kama moyo,unaosukuma maendeleo

Bila ya upendeleo,yapo mengi mafanikio

Amehaidi kwa kiapo,kuongoza kwa mfano

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi 

 

5.     Mengi yanatukumbusha awamu ile ya tano

Mikono kuchangamsha,uvivu kusema no

Hii inahamasisha,mingine yetu mitano

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi 

 

6.     Ushupavu ujasiri,ndio chake kipaumbele

Kawaweka mstari, Wanawake kifua mbele

Kusifika kwa mazuri, kwenye sekta  zote za mbele

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi 

 

7.     Wanawake tunaweza kusukuma hii dunia

Siku yetu tumeweza ,kutangaza yetu nia

Nyota tumeiangaza, bila ya kukata nia

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi 

 

8.     Kwa pamoja twaahidi, kushirikiana nawe

Kwa bidii na juhudi, kusimama nawe

Nyuma kamwe haturudi,kupingana nawe

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi 

 

9.     Muda nao si rafiki mmoja mwaka umepita

Ilani tumeiafiki,demokrasia imepita

Tena bila ya unafiki kwa Imani utapita

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi

 

10.  Kalamu naweka chini mama samia hongera

Tumuombee kwa Imani aliyetoka kwa dharura

Ameilinda yake Imani,kuitekeleza dhamira

Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi

 

Asante

                               Imeandaliwa na                             

 mwanamke

0714496369

Women innovators 4 Women Empowerment

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post