" WADAU WA ELIMU WATAKIWA KURIPOTI MATUKIO YA UKATILI

WADAU WA ELIMU WATAKIWA KURIPOTI MATUKIO YA UKATILI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala limewaomba wadau mbalimbali wa elimu kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia yanayowakumba wanafunzi wakati wakiwa mashuleni au majumbani kwao.

Wito huo umetolewa na Kamanda wa polisi  Mkoa wa Ilala ACP Debora Magiligimba leo tarehe 10/03/2022 katika kikao cha  wakuu wa shule za msingi na sekondari, na wadau wa elimu wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam katika ukumbi wa Anatogro - Dar es salaam.

Kamanda Magiligimba amewaomba kutenga muda wa kuzungumza na watoto ili kubaini ukatili wanaofanyiwa na wakaripoti katika sehemu husika ikiwemo madawati ya jinsia na watoto ambayo yapo katika wilaya zote za kipolisi mkoa wa Ilala. 

 "Chukueni muda wa kuongea na hawa watoto na muripoti matukio hayo katika sehemu husika ili kubaini aina ya ukatili wanaofanyiwa na kupata suluhisho ya matatizo hayo.

Ukatili huu unapelekea kumuathiri mtoto kisaikolojia na pia kupelekea kuathiri maendelea ya mtoto shuleni",amesema

Kikao hicho kiliandaliwa na chama cha walimu Tanzania halmashauri ya jiji la ilala na kuhudhuriwa na waratibu kata elimu sambamba na wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu wa shule za msingi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments