KANZIDATA YA TAIFA YA WANAWAKE NA UONGOZI TANZANIA YAZINDULIWA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akizindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amezindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden na Norway (Swedish International Development Cooperation Agency (Sida) and  Norwegian Agency for Development Cooperation -  Norad).


Uzinduzi huo umefanyika leo Jumanne Machi 8,2022 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kitaifa yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mongella amesema mfumo huo  ni kati ya nyenzo kubwa sana kwa ukombozi na kuleta usawa wa kijinsia kwa sababu wapo mabinti na wanawake wana sifa za kuwa viongozi kwa hiyo mfumo huo utasaidia sana.

“Niwapongeze wadau wote walioshiriki katika kutengenezwa kwa Kanzidata hii. Hongereni sana TGNP kwa kazi kubwa siku zote mmekuwa mstari wa mbele kuleta usawa wa kijinsia nchini. TGNP kazi zenu zinajulikana ni nzuri”,amesema Mongella.

Naye Mkurugenzi wa Jinsia, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwajuma Magwiza amewashukuru TGNP kwa kushirikiana Wizara kutengeneza mfumo huo ulioundwa na vijana wa Kitanzania ambao utasaidia katika upatikanaji wa taarifa za wanawake ili kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali amesema Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania ni mfumo rasmi wa kuhifadhi data mtandaoni ulioanzishwa ili kurekodi kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania walioko ndani na nje ya nchi.

Gemma amesema Mfumo huo una lengo la kuhifadhi kumbukumbu kuhusu wasifu wa wataalamu wanawake ili kurahisisha teuzi, mafunzo, kuchaguliwa nafasi mbalimbali pamoja na fursa mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi amesema Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania itarahisisha taarifa za ajira katika sekta ya Umma na sekta binafsi.

“Mfumo huu utawezesha Serikali pamoja na waajiri wa ndani na nje ya nchi kama vile taasisi za kuajiri na kuteua, kutafuta na kupata wanawake wa Kitanzania wenye ujuzi, weledi na ubobezi katika taaluma mbalimbali kwa ajili ya mitandao ya kitaalamu na kuchaguliwa katika nafasi zilizo wazi katika nyanja na sekta zote”,ameeleza Liundi.

Liundi amesema Tanzania ina wanawake wengi wenye uwezo wa kuongoza katika sekta mbalimbali hivyo amewahamasisha waajiri kutumia Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania ili kupata wanawake wenye sifa za uongozi.

“Ewe mwanamke karibu kujiunga katika Mfumo huu ili upate fursa mbalimbali kwa kutembelea Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi https://twl.jamii.go.tz Tunashauri wanawake kutumia mfumo huu kutoa taarifa zao (CV)”,amesema Liundi.

“Leo tumezindua Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania kinachofuata sasa ni kutekeleza mkakati wa kutangaza mfumo huu ili kuwafikia wanawake wengi zaidi. Mfumo huu ni wetu naomba tuutumie”,ameongeza.
Afisa Tehama Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu,Emiliana Clavery Nyarufunjo (kushoto) akielezea kuhusu Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad). Kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi amesema Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania akionesha anwani/Url  ya https://twl.jamii.go.tzya kuingia kwenye mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden (Sida) na Norway (Norad).
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).
Mkurugenzi wa Jinsia, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwajuma Magwiza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).
Mkurugenzi wa Jinsia, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwajuma Magwiza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akizindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).
Wadau wakipiga makofi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati)  kuzindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella akizungumza baada ya kuzindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania iliyoanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili  wa Wadau wa Maendeleo kutoka Sweden  (Sida) na Norway (Norad).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akipiga picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  baada ya kuzindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akipiga picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu baada ya kuzindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akipiga picha ya pamoja na wadau na wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  baada ya kuzindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella akipiga picha ya kumbukumbu na Viongozi wa TGNP baada ya kuzindua Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi, wa kwanza kulia ni Mwanachama wa TGNP, Jovitha Mlay akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali.
Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akionesha maandishi yanayosomeka Uzinduzi wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi
Kushoto ni Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akijadili jambo na Mwanachama wa TGNP Jovitha Mlay (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali (katikati) baada ya Uzinduzi wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi. 
Kushoto ni Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akifurahia jambo na Mwanachama wa TGNP Jovitha Mlay (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali (katikati) baada ya Uzinduzi wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo Machi 8,2022 jijini Arusha.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

 Soma pia :

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post