YANGA SC YAZIDI KUWA YA MOTO, YAONESHA UBABE MBELE YA MTIBWA SUGAR************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imeendelea kutoa dozi ligi ya NBC ambapo leo imeitembezea kichapo timu ya Mtibwa Sugar kwenye dimba la Manungu mkoani Morogoro.

Mabao ya Yanga Sc yamewekwa kimyani na mshambuliaji wao Said Ntibazokiza pamoja na Fiston Mayele ambaye mpaka sasa ana magoli 7 kwenye ligi.

Yanga sasa itaendelea kukaa kileleni mwa ligi kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya mpinzani wake Simba Sc.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post