DC MBONEKO ATEMBELEA UJENZI MRADI WA RELI YA KISASA SGR

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ametembelea kuona shughuli za maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano kutoka Mwanza hadi Isaka, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na wafanyakazi na kuzitafutia ufumbuzi, ambapo ujenzi huo unapita kwenye maeneo mbalimbali wilayani Shinyanga.


Mboneko amefanya ziara hiyo leo Februari 23,2022, akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya, pamoja na Naibu Meneja wa mradi wa Reli ya kisasa Mhandisi Alex Bunzu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo ambao unatekelezwa na Wakandarasi kutoka China.

Akizungumza kwenye ujenzi huo wa mradi wa Reli ya kisasa,Mboneko ameagiza vijana ambao wanatoka kwenye maeneo husika mradi ambapo unapopita wapatiwe ajira, na siyo kupewa vijana kutoka maeneo mengine.

“Mradi huu wa ujenzi wa Reli ya kisasa ujenzi unachukua muda wa miaka mitatu kukamilika, hivyo tunataka wananchi wa maeneo husika ambao wanapitiwa na mradi huu wanufaike nao ikiwamo  vijana kupata ajira, na siyo kupewa ajira vijana kutoka maeneo mengine na wakati eneo hilo la mradi kuna vijana wengi na hawana ajira,”alisema Mboneko.

“Na nyie vijana ambao mmepata ajira kwenye mradi huu wa Reli ya kisasa hasa madereva acheni wizi, sababu kumekuwa na wimbi kubwa sana la wizi wa mafuta, huko ni kuhujumu mradi huu, na ninatoa onyo la mwisho mkiiba tena mafuta tunafukuza kazi madereva wote,”aliongeza.

Alisema pia Madereva wanapokuwa wakiiba mafuta hayo na kuwauzia wananchi na kutunza ndani ya nyumba zao ni kutengeneza janga jingine, ambalo linaweza kusababisha maaafa makubwa kwa wananchi kulipukiwa na mafuta hayo.

Aidha Mboneko, aliagiza  wananchi ambao bado hawajalipwa Fidia waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa Reli ya kisasa walipwe wote pesa zao, na kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa hakuna ambaye hatalipwa pesa yake ya Fidia bali wote watalipwa, huku akiwataka pesa hizo wazitumie kwa maendeleo ikiwamo kujenga nyumba bora.

Katika hatua nyingine Mboneko aliagiza suala la mikataba mibovu ya wafanyakazi litafutiwe ufumbuzi wa haraka, pamoja na upewaji wa chakula bora na cha uhakikisha ili kutodhoofisha Afya za wafanyakazi.

Pia aliagiza ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya wafanyakazi wa Mradi huo wa Reli ya kisasa zijengwe kwa kasi inayotakiwa na kwa kuzingatia ubora, huku akiwataka wanawake ambapo mradi huo unapita wachangamkie fursa ya kuuza vyakula kwenye ujenzi huo na kupata pesa.

Kwa upande wake Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, alisema maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya watayafanyia kazi, likiwamo suala hilo la ulipwaji wa Fidia, na upewaji wa mikataba mizuri, huku akibainisha kuwa pia kuna kamati ilishaundwa ambayo itapita kukusanya maoni na malalamiko ya wafanyakazi na kutafutiwa ufumbuzi.

Bunzu aliwataka pia vijana ambao wanafanyakazi kwenye ujenzi huo wa Reli ya kisasa, wawe wazalendo na nchi yao na kuacha tabia ya wizi wa vitu mbalimbali, ambapo kumekuwa na wizi mkubwa sana, huku akisema mradi huo utakamilika 2024 wenye gharama ya Sh.Trilioni 3.062.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisikiliza malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Maskati wilayani humo, ambao wanapitiwa na mradi wa Reli ya kisasa (SGR) ambapo walikuwa wakidai hawajalipwa fidia na ukosefu wa ajira kwa vijana wao, na kuahidi kutatua malalamiko yao yote.

Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya na kuahidi changamoto zote zitafanyiwa kazi.

Baadhi ya wafanyakazi katika mradi huo wa Reli ya kisasa, wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko juu ya utatuzi wa malalamiko yao.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na Wakandarasi ambao wanatekeleza mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano, na kuwataka wazingatie maelekezo ya ajira na kufuata sheria za nchi, pamoja na kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea na ukaguzi wa maendeleo ujenzi wa Reli ya kisasa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (wapili kushoto) akisikiliza maelezo ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya wafanyakazi wa Reli hiyo ya kisasa (SGR), ambazo zipo Luhumbo wilayani Shinyanga, akitoa maelezo hayo ni Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akiwa na Naibu Meneja wa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, akikagua ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi huo wa Reli ya kisasa.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments