WABUNGE WA CCM WAMPITISHA ZUNGU KUGOMBEA UNAIBU SPIKA


Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempitisha Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Spika wa Bunge, jijini Dodoma, leo Jumanne Februari 8, 2022.

Zungu amepitishwa na wabunge wote wa CCM baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kupitisha jina lake pekee kati ya wabunge 11 wa chama hicho waliokuwa wakiomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya jina lake kupitishwa Zungu amewashukuru wabunge wa chama chake kwa kumpa kura za kishindo na ameahidi kushirikiana na wabunge wenzake endapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika Februari 11, 2022.

Amesema jukumu lake litakuwa ni kutekeleza maagizo ya Spika wa Bunge kwa kuwa ndiye bosi wake wa kwanza ndani ya Bunge.


"Ninamshukuru Mungu muumba wa mbingu na nchi na  Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwenyekiti wa CCM yeye na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wote kwa kurudisha jina langu na kupigiwa kura na wabunge upande wa Chama cha Mapinduzi", amesema Zungu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post