MKULIMA ALIYEOKOTA FURUSHI LENYE MAMILIONI YA FEDHA AKITOKA SHAMBANI ARUDISHA KWA MWENYEWE



Nchini Benin, mkulima mtaalamu amepokea tuzo ya heshima kutoka kwa mamlaka ya nchi yake.

 Alimrudishia mmiliki wake kiasi cha mamilioni ya fedha zilizokuwa kwenye begi la kusafiria alilolichukua alipokuwa njiani Ijumaa iliyopita alipokuwa akirejea kutoka shambani kwake.

Baraka Amidou ana umri wa miaka 37. Ameoa na baba wa watoto 5. Alipowasiliana na BBC Afrique, alitufanya tuwasiliane na mpwa wake Soule Mohamed Taïrou ili awe mkalimani kwa sababu hazungumzi Kifaransa.


Kuhusu uamuzi wake wa kurejesha fedha hizo, anasema ulichochewa na imani na malezi ya kidini na anasema wala hajutii alichokifanya.


Alitunukiwa cheti cha kutambuliwa na bahasha ya fedha. Kwa mujibu wa mamlaka, ni suala la kumtia moyo na kutambua kitendo chake cha uadilifu.


"Siku hizi tunazidi kushuhudia upotevu wa maadili. Haijapata kutokea kijana ambaye bado ana kila kitu cha kufanya ili kujijenga akafanya kitendo kama hicho. Haya yalitangazwa na Djibril Mama Cissé, Gavana wa Borgou kaskazini mwa Benin.


Aliokota begi alipokuwa akirudi kutoka shambani kwake. Baada ya kusikia kupitia tangazo la mjini kwamba mwenye nyumba alikuwa akitafuta mfuko huo, alienda kuukabidhi kwa chifu wa kijiji chake.


Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, begi hilo ni la mfanyabiashara aliyefika kununua nafaka mkoani humo.


Amidou Baraka alikataa CFA 100,000 ambayo mmiliki alitaka kumpa ili kumshukuru. Baada ya kusisitiza, hatimaye alikubali kupokea 50,000 FCFA.


Hadithi inayokumbusha ile ya Mliberia Emmanuel Tolué, dereva wa pikipiki ambaye aliokota na kurejesha dola za Marekani 50,000, au zaidi ya faranga za CFA milioni 28.


Rais wa Liberia George Weah alikutana naye katika sherehe katika mji mkuu Monrovia na kumpa pesa na kumsomesha.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

  1. Naam haqqan, hayo ndo mafundisho ya uislam,mtume Muhammad swala llahu alayhi wasallam katufundisha "mwenye kuacha kufanya jambo la haramu kwa kumuogopa Allah , basi Allah atampa badali ya hicho kilicho bora zaidi kwa njia ya halali"
    Hivyo atarajie kupata mbadala wa hicho alicho kirejesha kwa njia ya halali,

    ReplyDelete

Post a Comment