MWANAMKE ANYONGWA NYUMBANI KWAKE GEITA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe

Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linaendelea na uchunguzi kufuatia tukio la mauaji ya mke wa mfanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa GGM aliyefahamika kwa jina la Anjela Anteli mwenye umri wa miaka 43, aliyekutwa amenyongwa nyumbani kwake jana Februari Mosi, 2022, majira ya saa 8:00 mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Februari 2, 2022 Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Majengo, Kata ya Kanyara, Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo mtu wa kwanza kugundua tukio hilo alikuwa ni bodaboda ambaye aliagizwa kupeleka maziwa nyumbani hapo na alipofika akagonga mlango bila mafanikio.


Kamanda Mwaibambe, amesema kuwa mtu wa kwanza kugundua alikuwa bodaboda ambaye aliagizwa kupeleka maziwa nyumbani hapo na alipofika akagonga mlango bila mafanikio.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments