Tazama Picha : TAMASHA LA "DON BOSCO DIDIA SPORTS DAY 2022"


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali waliyoiandaa katika tamasha la "Don Bosco Didia Sports Day 2022"

Na Mwandishi wetu-Malunde1 blog

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga wamefanya tamasha la michezo waliloliita "Don Bosco Didia Sports Day 2022"

Akizungumza katika Tamasha hilo, Februari 19, 2022Mwalimu wa michezo wa shule hiyo James Karioki maarufu kwa jina la Zipapa,amesema Tamasha hilo huwa linafanyika kila mwaka mwezi wa pili au wa tatu kulingana na hali ya hewa.

Amesema kwa mwaka huu  tamasha hilo limehusisha michezo mingi na wanafunzi walijiandaa kwa muda wa wiki mbili ambapo uzinduzi ulifanyika Februari 5, 2022 kwa Mbio za riadha lengo likiwa ni kuibua vipaji, kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuviendeleza vipaji vya wanafunzi wao waweze kushiriki michezo kitaifa na kimataifa.

"Tunaamini michezo ni Ajira, ndiyo maana katika shule yetu tunahakikisha vijana wetu wasipofaulu kwa upande wa taaluma ya darasani basi kwenye michezo watafaulu ili washiriki michezo inayoandaliwa duniani kote na katika mashindano haya mipira huwa tunaiweka pembeni", amesema Zipapa.

Ameitaja baadhi ya michezo iliyofanyika katika mashindano ya tamasha la "Don Bosco Didia Sports Day 2022" kuwa ni pamoja na mbio za mita 100,200,400 na 800,mbio za vijiti,mbio za baiskeli,kurusha mkuki,kuruka kamba,kuruka umbali mrefu,mbio za kuendesha baiskeli taratibu,wheel barrow race,three legend race,obstacle race,skiping,tripple jump na tag of war.

Ameeleza hadi kufanikisha tamasha hilo waliwagawa wanafunzi katika makundi manane ambayo ni Kilimanjaro,Manyara,Meru,Ngorongoro,Ruaha,Serengeti,Tanganyika na Victoria.

Akitaja baadhi ya washindi amesema,katika mchezo wa kuvuta kamba washindi ni Kundi la Kilimanjaro boys na Ngorongoro girls,mbio za baiskeli mshindi kwa upande wa wavulana ni Paschal Sasagu na kwa upande wa wasichana mshindi ni Bernadeta Nzungu.

Kwa upande wa Riadha washindi ni Baraka Clement,Rahel Juma,Enock Peter na Anwarite Alex,kupamba maturubai washindi ni kundi la Tanganyika,mchezaji bora kwa upande wa wavulana ni Enock Making nakwa upande wa wasichana ni Aplonia Elias na Washindi wa jumla nafasi ya kwanza ni kundi la Victoria,nafasi ya Pili Serengeti na nafasi ya tatu ni Ngorongoro.

Naye Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo ambaye ni -Afisa Ushirikishwaji Jamii Wilaya ya Shinyanga, ASP Osward Patric Nyorobi amesema amejifunza mengi kupitia tamasha hilo na amefurahi kuona shule ya Don Bosco sekondari Didia inafundisha Uzalendo na ukakamavu,hivyo ametoa rai kwa shule zingine za wilaya ya shinyanga waige namna Don bosco wanafanya angalau watenge wiki moja kwa ajili ya michezo tu kwa sababu michezo ni ajira.

Tazama picha hapa chini..
Mgeni Rasmi Afisa Ushirikishwaji Jamii Wilaya ya Shinyanga ASP Osward Patric Nyorobi  akizungumza katika tamasha la "Don Bosco Didia Sports Day 2022"
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia Fr. Vicent Mokaya akizungumza katika tamasha la "Don Bosco Didia Sports Day 2022"
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia Sista Magdalene Mativo akishiriki mbio za Baiskeli katika tamasha la "Don Bosco Didia Sports Day 2022"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments