MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AFARIKI BAADA YA 'JOGOO' WAKE KUWIKA SIKU TATU MFULULIZO


Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha Maasai Mara ameaga dunia baada ya jogoo wake kuwika kwa siku tatu mfululizo katika Kaunti ya Narok nchini Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mwanafunzi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 22 alifariki akiwa katika Hospitali ya Shepherd alikokuwa amelazwa akipokea matibabu baada ya kulalamikia maumivu kwenye eneo lililo chini ya tumbo yake na jogoo wake kuwika bila kukoma

 Tukio hilo liliripotiwa na Msimamizi wa Maslahi ya Wanafunzi Chuoni humo Aden Mohamed aliyesema kuwa mwendazake alikuwa ameshuhudia jogoo wake akiwika kwa siku tatu bila kukoma.

 Jogoo huyo aliwika kutoka Jumamosi, Februari 19 hadi Jumatatu, Februari 21,2022 na kuufanya usimamizi wa chuo hicho kumpeleka hospitalini.

“Kuna mwili wa mwanafunzi katika Hospitali ya Shepherd aliyelazwa Februari 23 mwendo wa saa 10:20 asubuhi akilalamikia maumivu chini ya tumbo na jogoo wake kuwika bila kukoma tangu Jumamosi Februari 19,” ripoti ya polisi inasema. 

Maafisa wa polisi walizuru hospitali hiyo na kumtambua mwanafunzi huyo ambaye alikuwa amehudhuria hafla moja ya sherehe na wenzake watano mnano Februari 18.

 Inadaiwa kuwa punde tu baada ya kupata mlo, mwanafunzi huyo alianza kulalamika kuhusu jogoo wake kuwika bila kukoma hali iliyomlazimu kutafuta matibabu.

 “Mwili ulipigwa picha na maafisa wa eneo la tukio Narok na kupelejwa katika makafani ya Hospitali ya Rufaa ya Narok ukisubiri kufanyiwa upasuaji,” ripoti hiyo iliongeza. 

Maafisa kutoka kwa Idara ya Upelelezo wa Jinai (DCI) tawi la Narok Kaskazini wanashughulikia suala hilo kwa lengo la kubaini mazingira na chanzo cha kifo hicho.

Chanzo- Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post