" RAIS SAMIA : JOSHUA NASSARI ALIKUWA ANATUCHACHAFYA BUNGENI

RAIS SAMIA : JOSHUA NASSARI ALIKUWA ANATUCHACHAFYA BUNGENIKushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Nassari, kulia ni Rais Samia Suluhu Hassan.
**
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu, Februari 7, 2022 akiwa kwenye ziara Mkoani Mara amesema anashukuru kwamba taarifa zilizomfikia kuhusu utendaji wa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Joshua Nassari ni za kumsifia kazi anayoifanya ndani ya Wilaya hiyo.

“Wale wote tuliowaamini nataka niwaombe mfanye kazi yenu vema, kwa Wananchi nimewaletea Wakuu wa Wilaya wachangaaachanga ili waweze kwenda mbio ombi langu waungeni mkono msiwapige vita.

“Na nashukuru Joshua Nassari ( DC wa Bunda) amesifiwa sana hapa, kwa wasiomjua Nassari alikuwa anatuchachafya Bungeni kule lakini aliposema nimesalimu amri naungana na nyie siwezi kushinda na nyie na mie nikamwambia yale uliyokuwa unayasema Bungeni kayatekeleze na mtihani wako wa kwanza nakupeleka Mara nenda katekeleze huko nashukuru nimesikia unafanya vizuri,” amesema Rais Samia leo akiwa mkoani Mara.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments