WAWILI WAJERUHIWA KWA RADI 'WAKI - CHAT KWA SIMU' MVUA KUBWA IKINYESHA ARUSHA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo 

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Watu wawili wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kupigwa na radi wakichunga mifugo katika kitongoji cha Olodonyokeri kijiji na kata ya Olosokokwani wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha huku chanzo kikidaiwa na kutumia simu 'kuchat' wakati mvua kubwa ikinyesha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema tukio hilo limetokea Februari 17,2022 saa  9 alasiri na kuwataja waliojeruhiwa na radi hiyo ni Sasines Onarok Babu (25) mkazi wa Olosokokwani na mwingine ni Kishuyan Terya Kiyomi (28) na walikimbizwa katika zahanati ya kijiji cha Ololosokwani na kupatiwa matibabu.

"Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni matumiziya simu wakati mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kuambatana na radi ambayo ilipelekea vijana hao kujeruhiwa sehemu mbalimbali ya miili yao na radi hiyo",amesema Kamanda Masejo.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari hasa kipindi cha mvua kubwa ambazo huambatana na radi kali huku akiwataka kuacha mara moja matumizi ya vifaa vya umeme ikiwemo simu wakati wa mvua kwani kwa kufanya hivyo kutawaepusha na madhara makubwa yanayoweza kutokea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post