AMUUA MUME KWA KUMCHOMA KISU MARA 140


Joan Burke

Mwanamke mmoja anayeitwa Joan Burke (61), kutoka jimbo la Florida nchini Marekani, ameshtakiwa kwa mauaji kufuatia tuhuma za kumchoma na kisu mume wake kwa zaidi ya mara 140 na kupelekea kifo chake.

Kwa mujibu wa polisi kutoka kituo Palm Springs, walisema kwamba walipokea simu mnamo Februari 11, 2022, kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama ni mtoto wa mtuhumiwa baada ya kufika nyumbani na kukuta mwili wa baba yake wa kambo Melvin Weller (62) ukiwa chini na umezungukwa na damu nyingi, na ndipo maafisa wa polisi walipofika eneo la tukio.

Kufuatia uchunguzi wa madaktari uliofanywa kwenye mwili wa mwanaume huyo ulibaini kwamba alipata zaidi ya majeraha 140 ya kuchomwa na kuvunjika kwa fuvu la kichwa baada ya kupigwa na kisu cha nyama.

Chanzo : BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments