MWANAMKE AKABIDHI MTOTO KISHA KUJINYONGA NDANI YA GESTI YA MUME WAKE 'MWANANZOKA'

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa Mji mdogo wa Katoro Wilayani Geita amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Mwananzoka inayomilikiwa na mumewe Siki Mwananzoka.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi Februari 3,2022 majira saa 12 jioni baada ya marehemu akiwa na mtoto mchanga wa miezi 4 kumkabidhi mtoto huyo kwa mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni na baada ya masaa 4 aligundulika akiwa amefariki duhia baada ya kukutwa akiwa amejining’iniza kwa kamba iliyodaiwa kufungwa juu ya dali chooni.

Mhudumu wa nyumba hiyo ya wageni iliyopo Katoro mjini Monica Paulo amesema mke wa mwajiri wake, alifika kwenye nyumba hiyo majira ya saa 8 mchana na kumtaka amsaidie kubeba mtoto akapumzike akidai hajisikii vizuri kiafya.

Monica ameeleza kuwa marehemu aligundulika baada ya Mteja mmoja kufika na kuomba huduma huduma ya choo na akakuta mtu kajinyonga chooni.

Kiongozi wa eneo hilo Stephano Bandola amekiri kutokea kwa tukio na kufafanua kuwa chanzo cha tukio hilo kinaweza kuwa ni migogoro ya kufamilia.

Imeelezwa kuwa wakati tukio hilo kukitokea,mume wa marehemu alikuwa safarini.

 Chanzo : MwangazaTV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post