SABABU KIFO CHA MWELE MALECELA


BAADA ya kusambaa kwa taarifa za kusikitisha kuhusu aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele, Dk. Mwele Ntuli Malecela kufariki dunia, jana Alhamisi, Februari 10, 2022, Geneva mchini Uswisi, familia ya marehemu imetaja chanzo cha kifo hicho.

Kaka wa Marehemu William Malecela maarufu kama Lemutuz amesema kifo cha dada yake kimesababishwa na kansa.

“Ni kweli amefariki leo Hospitalini Geneva, Switzerland alikua anasumbuliwa na Kansa, msiba utakuwa Dodoma,” amesema Lemutuz.

Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post